Hatimaye Hukumu Shambulio la Westgate Kutolewa

October 5, 2020

MAHAKAMA moja nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi inayohusisha wanaume watatu walioshtakiwa kwa kuwasaidia wanamgambo wenye silaha kushambulia jengo la manunuzi katika mji mkuu wa Nairobi, mwaka 2013.

Takriban watu 67 waliuawa katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa katika jumba la manunuzi la Westgate.

Wanamgambo wa Kiislamu wenye makao yao nchini Somalia walikiri kutekeleza shambulizi hilo. Aidha serikali ilisema kwamba wanamgambo waliotekeleza shambulizi hilo waliuawa.

Zaidi ya watu 140 walitoa ushahidi kwenye kesi hiyo ambapo washitakiwa walikanusha kufanya njama ya kutekeleza ugaidi.

Kutolewa kwa hukumu kutahamasisha nchi ambayo bado ipo katika tahadhari ya juu kwa uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi, na ambayo jeshi lake bado liko nchini Somalia kukabiliana na vikosi vya al-Shabab kutoka kwenye kambi zao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *