Harmonize anunua ugomvi wa Alikiba “Upo tayari kwa mfalme wa mafundo”,

October 1, 2020

Kama umeusikiliza wimbo mpya wa Alikiba ‘Mediocre’ kuna sehemu amewapiga dongo wapinzani wake kwa kusema “Pluu mpaka chini pigo, unataka u-king na mafundo mimi ndiyo baba Kingdom tena mnaji-show huyu Komando stage mafundo”.

Fumbo hilo linatafsirika kama ni dongo kwenda kwa mtoto wa jirani na msanii Harmonize kwa sababu anatumia jina Jeshi, pia alitumia njia ya kushuka kama Komando kwenye siku ya utambulisho wa wachezaji wapya wa klabu ya Yanga.

Sasa kupitia post aliyoweka Harmonize kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram amempost msanii wake Ibraah Tz kisha akamjibu Alikiba kwa kuandika “Upo tayari kwa mfalme wa mafundo”.

Mashabiki wengi wame-comment picha hiyo kwa kusema kama anatumia kiki ya Alikiba ili watu kumpa ‘attension’ msanii wake, huku wengine wanasema kwamba hajaimbwa ila amedakia ugomvi wa watu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *