Harmonize afungiwa safari kutoka Musoma mpaka DSM

October 8, 2020

 

EATV & EA Radio Digital, imefanya mahojiano na dada aliyejitambulisha kwa jina la Victoria Romanus ambaye ametoka Mkoani Musoma hadi Dar Es Salaam kwa lengo la kumuona na kutaka kufanya kazi ya uchezaji kwa msanii Harmonize.

Victoria Romanus amesema yeye ni mgeni, na Dar Es Salaam amefikia maeneo ya Mbagala Mission kwa shangazi yake, hivyo anafanya kazi ya kuzunguka kwenye vyombo vya habari ili kupata msaada wa kuonana na Harmonize.

“Mimi nina kipaji cha sanaa ya uchezaji, nimetoka Musoma kuja Dar Es Salaam kwa dhumuni moja tu la kumtafuta Harmonize kwa sababu napenda kuwa mchezaji wake, kwa upande wa kutafuta nauli nilihangaika sana mama yangu alikuwa hana uwezo wa kunipa nauli, hivyo nikawa natunza pesa zangu mwenyewe huku nikifanya shughuli ndogondogo kwa mwezi mmoja ili nipate nauli ya kuja huku kumpata Harmonize” ameeleza 

Dada huyo hakuishia hapo kwani amefikia hatua ya kumwaga machozi kwa uchungu huku akisema anampenda sana Harmonize kuliko wasanii wote pia ndiyo shabiki yake mkubwa japo anakatishwa tamaa na watu kwamba hawezi kumpata msanii huyo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *