Hans Poppe: Nasubiria hukumu kutoka TFF, on September 19, 2020 at 7:00 am

September 19, 2020

 MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Zacharia Hans Poppe ameshangaa kuona hadi leo Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), haijampa barua ya hukumu yake ya kutakiwa kulipa faini ya milioni tano.Hans Poppe, Msemaji wa Simba, Haji Manara na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bombuli wamejikuta wakikumbwa na rungu la Kamati ya Maadili kwa kufanya makosa mbalimbali wakati wa hukumu ya Bernad Morrison.Kwa upande wa Hans Poppe amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na makosa mawili aliyoyafanya, moja likiwa ni kutoa taarifa ya shauri ambalo lilikuwa likisikilizwa huku yeye akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, pili kutoa maneno ya kiuchochezi kwa umma.Akizungumza na Championi Ijumaa, Hans Poppe amesema kuwa, anashangaa kuona hadi leo ‘juzi’ hajapatiwa barua ya hukumu yake na badala yake amekuwa akisikia masuala hayo kupitia wanahabari na kudai kuwa mara baada ya kuipata barua hiyo ataichambua na ili kujua kigezo kilichotumika.“Bado hawajanipatia barua yoyote hadi sasa kutokana na maamuzi yaliyofanyika ya kupewa adhabu, siwezi kuchukua maamuzi yoyote, nimesikia maneno kutoka kwenu, wao walivyoniita awali kwenda kujieleza, walijua ni jinsi gani walinipata hadi nikaenda kwenye kile kikao chao na kutoa maelezo.“Kwa nini wasinipe hukumu yao kupitia njia ileile ambayo waliitumia kuniita, kwa nini wasiniletee barua ya maamuzi waliyoyafanya na wanakaa kimya hadi leo au ni maneno tu yanatungwa.“Nikiipata hiyo barua ndio nitajua vigezo gani vimetumika kunipa hukumu hiyo kwa sababu kama sijaridhika na maamuzi yao lazima nikate rufaa kwa sasa sielewi maelezo yao yakoje,” alisema Hans Poppe.,

 

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Zacharia Hans Poppe ameshangaa kuona hadi leo Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), haijampa barua ya hukumu yake ya kutakiwa kulipa faini ya milioni tano.

Hans Poppe, Msemaji wa Simba, Haji Manara na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bombuli wamejikuta wakikumbwa na rungu la Kamati ya Maadili kwa kufanya makosa mbalimbali wakati wa hukumu ya Bernad Morrison.

Kwa upande wa Hans Poppe amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na makosa mawili aliyoyafanya, moja likiwa ni kutoa taarifa ya shauri ambalo lilikuwa likisikilizwa huku yeye akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, pili kutoa maneno ya kiuchochezi kwa umma.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Hans Poppe amesema kuwa, anashangaa kuona hadi leo ‘juzi’ hajapatiwa barua ya hukumu yake na badala yake amekuwa akisikia masuala hayo kupitia wanahabari na kudai kuwa mara baada ya kuipata barua hiyo ataichambua na ili kujua kigezo kilichotumika.

“Bado hawajanipatia barua yoyote hadi sasa kutokana na maamuzi yaliyofanyika ya kupewa adhabu, siwezi kuchukua maamuzi yoyote, nimesikia maneno kutoka kwenu, wao walivyoniita awali kwenda kujieleza, walijua ni jinsi gani walinipata hadi nikaenda kwenye kile kikao chao na kutoa maelezo.

“Kwa nini wasinipe hukumu yao kupitia njia ileile ambayo waliitumia kuniita, kwa nini wasiniletee barua ya maamuzi waliyoyafanya na wanakaa kimya hadi leo au ni maneno tu yanatungwa.

“Nikiipata hiyo barua ndio nitajua vigezo gani vimetumika kunipa hukumu hiyo kwa sababu kama sijaridhika na maamuzi yao lazima nikate rufaa kwa sasa sielewi maelezo yao yakoje,” alisema Hans Poppe.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *