Hamissa Mobeto: Diamond Platnumz ni Wangu Milele

September 7, 2020

VIPI aongeze sauti? Hamisa Mobeto ndiyo ameshasema kwamba, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi, ni wake wa milele.Akipiga stori juzikati na Risasi Jumamosi, jijini Dar es Salaam, Mobeto ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali alisema anaanzaje kujiweka kando na Mondi ambaye ni baba wa mtoto wake?“Sijui kwa nini naulizwa mambo ya Mondi kila siku, labda kuna kitu watu wanataka kukisikia kutoka kwangu kuhusu Diamond. “Huyu ni mzazi mwenzangu, tunalea mtoto wetu vizuri hakuna shida kati yetu, Diamond ni wangu wa milele,” alisema Mobeto.WANAOKEREKA SHAURI YAOKauli hii huwenda ikawakera wengi, hasa wale waliopita anga za Mondi kwenye suala la uhusiano wa kimapenzi, lakini Mobeto amesema: “Mwenye kununa na anune, shauri yake.”Aidha, mwandishi wetu alipomuuliza mwanamitindo huyo kuhusu uhusiano wake na Tanasha Donna na Zarinah Hassan, ambao nao wamezaa na Mondi, alisema: “Nawapenda wote.“Wewe mwenyewe unaona tuko karibu na Tanasha, tunashauriana kwa mengi na kuendesha harakati za kusaka fedha.“Hata Zari mimi sina tatizo naye, mimi natamani sisi wote tuwe kitu kimoja kwa sababu tumezaa na Diamond, tumeshatengeneza ukoo.“Kama watoto wetu ni familia moja, kwa nini sisi tuishi kwa kuchukiana?Tunataka na watoto wetu waje wachukiane?Mimi sioni kama hili ni jambo zuri.MOBETO NI MKE MTARAJIWA?Mwanamitindo huyo alipoulizwa kwamba yeye ndiye chaguo la Mondi kama mke mtarajiwa, alisema suala la kuoa liko kwa Diamond na kutaka aulizwe yeye.“Diamond si unamfahamu, muulize yeye nani ni mke wake mtarajiwa, usiniulize mimi.”HABARI ZA UMBEYAKatika siku za hivi karibuni, kumekuwa na habari za umbeya kuwa Mobeto na Mondi wako kroz, kiasi cha kuwafanya watu ‘wagesi’ kwamba, huwenda penzi lao limekolea upya.Hivi karibuni Mobeto alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa, alihusika kumshonea nguo mzazi mwenzake huyo, ambazo alizivaa kwenye uzinduzi wa EP ya Zuhura Othman ‘Zuchu’ uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar, Julai 18, mwaka huu.Hata hivyo, wapo wanaojiongeza zaidi na kusema kwamba, Mobeto na Mondi siku hizi ni kama wanapika na kupakua, jambo ambalo wahusika hawajalithibitisha.MKE MTARAJIWA WA MONDI PASUA KICHWATangu Mondi atangaze kuwa mwaka huu lazima ‘avute jiko’, mkewe mtarajiwa amekuwa pasua kichwa kwa wachunguza mambo ya wengine.Miruzi imekuwa mingi huku wanawake kadhaa wakitajwa kuwepo kwenye tageti za Mondi, ambao ni Zuchu, Mobeto na mwanamke mmoja kutoka Rwanda, anayetajwa kwa jina la Shaddy Boo.Hata hivyo, mara kadhaa Mondi anapoulizwa kuhusu mtarajiwa wake, anaishia kusema: “Atafahamika muda ukifika.”Uchunguzi wa Risasi mitandaoni, ambao siku hizi mikeka ya umbeya hutandikwa huko kwa wingi, umebaini kuwa mashabiki wengi wa msanii huyo, wanavoti kura zao kwa Zari.Zari ambaye ni raia wa Uganda, amezaa watoto wawili na Mondi, ambao ni Tiffah na Nillan. Aidha, wengine wamemshauri msanii huyo kumuoa Mobeto, aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Dillan, huku wengine wakimpigia debe Zuchu avae heshima ya kuitwa mke wa Diamond.Kura za Tanasha mara nyingi zimekuwa chache, ingawa wapo wanaomtaka Mondi amuoe mwanamke huyo raia wa Kenya, aliyezaa naye mtoto mmoja ajulikanaye kwa jina la Naseeb Junior. Shaddy anayetajwa kuwa ni mtoto kutoka familia ya kitajiri, hajasemwa sana mitandaoni, kutokana na habari zake kutoshika kurasa nyingi za udaku.UAMUZI NI WA MONDIWaswahili husema, kelele za chura hazizuii maji kutekwa; ni wazi kwamba yote yanayosemwa kuhusu mke mtarajiwa wa Mondi, ni ushauri tu kwake, ila uamuzi unabaki mikononi mwa muoaji.Siku inayotajwa kuwa ya kipekee, ni Oktoba 2, mwaka huu ambapo mbali na Mondi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza umri wa miaka 31, inatajwa pia kuwa huwenda msanii huyo akafunga ndoa.Subira yavuta heri, cha kuomba uzima ili tarehe hiyo ifike na watu washuhudie ndoa ya staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva iliyosubiriwa na watu wengi kwa hamu.,

VIPI aongeze sauti? Hamisa Mobeto ndiyo ameshasema kwamba, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi, ni wake wa milele.

Akipiga stori juzikati na Risasi Jumamosi, jijini Dar es Salaam, Mobeto ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali alisema anaanzaje kujiweka kando na Mondi ambaye ni baba wa mtoto wake?

“Sijui kwa nini naulizwa mambo ya Mondi kila siku, labda kuna kitu watu wanataka kukisikia kutoka kwangu kuhusu Diamond. “Huyu ni mzazi mwenzangu, tunalea mtoto wetu vizuri hakuna shida kati yetu, Diamond ni wangu wa milele,” alisema Mobeto.

WANAOKEREKA SHAURI YAO

Kauli hii huwenda ikawakera wengi, hasa wale waliopita anga za Mondi kwenye suala la uhusiano wa kimapenzi, lakini Mobeto amesema: “Mwenye kununa na anune, shauri yake.”

Aidha, mwandishi wetu alipomuuliza mwanamitindo huyo kuhusu uhusiano wake na Tanasha Donna na Zarinah Hassan, ambao nao wamezaa na Mondi, alisema: “Nawapenda wote.

“Wewe mwenyewe unaona tuko karibu na Tanasha, tunashauriana kwa mengi na kuendesha harakati za kusaka fedha.

“Hata Zari mimi sina tatizo naye, mimi natamani sisi wote tuwe kitu kimoja kwa sababu tumezaa na Diamond, tumeshatengeneza ukoo.

“Kama watoto wetu ni familia moja, kwa nini sisi tuishi kwa kuchukiana?

Tunataka na watoto wetu waje wachukiane?

Mimi sioni kama hili ni jambo zuri.

MOBETO NI MKE MTARAJIWA?

Mwanamitindo huyo alipoulizwa kwamba yeye ndiye chaguo la Mondi kama mke mtarajiwa, alisema suala la kuoa liko kwa Diamond na kutaka aulizwe yeye.

“Diamond si unamfahamu, muulize yeye nani ni mke wake mtarajiwa, usiniulize mimi.”

HABARI ZA UMBEYA

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na habari za umbeya kuwa Mobeto na Mondi wako kroz, kiasi cha kuwafanya watu ‘wagesi’ kwamba, huwenda penzi lao limekolea upya.

Hivi karibuni Mobeto alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa, alihusika kumshonea nguo mzazi mwenzake huyo, ambazo alizivaa kwenye uzinduzi wa EP ya Zuhura Othman ‘Zuchu’ uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar, Julai 18, mwaka huu.

Hata hivyo, wapo wanaojiongeza zaidi na kusema kwamba, Mobeto na Mondi siku hizi ni kama wanapika na kupakua, jambo ambalo wahusika hawajalithibitisha.

MKE MTARAJIWA WA MONDI PASUA KICHWA

Tangu Mondi atangaze kuwa mwaka huu lazima ‘avute jiko’, mkewe mtarajiwa amekuwa pasua kichwa kwa wachunguza mambo ya wengine.

Miruzi imekuwa mingi huku wanawake kadhaa wakitajwa kuwepo kwenye tageti za Mondi, ambao ni Zuchu, Mobeto na mwanamke mmoja kutoka Rwanda, anayetajwa kwa jina la Shaddy Boo.

Hata hivyo, mara kadhaa Mondi anapoulizwa kuhusu mtarajiwa wake, anaishia kusema: “Atafahamika muda ukifika.”

Uchunguzi wa Risasi mitandaoni, ambao siku hizi mikeka ya umbeya hutandikwa huko kwa wingi, umebaini kuwa mashabiki wengi wa msanii huyo, wanavoti kura zao kwa Zari.

Zari ambaye ni raia wa Uganda, amezaa watoto wawili na Mondi, ambao ni Tiffah na Nillan. Aidha, wengine wamemshauri msanii huyo kumuoa Mobeto, aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Dillan, huku wengine wakimpigia debe Zuchu avae heshima ya kuitwa mke wa Diamond.

Kura za Tanasha mara nyingi zimekuwa chache, ingawa wapo wanaomtaka Mondi amuoe mwanamke huyo raia wa Kenya, aliyezaa naye mtoto mmoja ajulikanaye kwa jina la Naseeb Junior. Shaddy anayetajwa kuwa ni mtoto kutoka familia ya kitajiri, hajasemwa sana mitandaoni, kutokana na habari zake kutoshika kurasa nyingi za udaku.

UAMUZI NI WA MONDI

Waswahili husema, kelele za chura hazizuii maji kutekwa; ni wazi kwamba yote yanayosemwa kuhusu mke mtarajiwa wa Mondi, ni ushauri tu kwake, ila uamuzi unabaki mikononi mwa muoaji.

Siku inayotajwa kuwa ya kipekee, ni Oktoba 2, mwaka huu ambapo mbali na Mondi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza umri wa miaka 31, inatajwa pia kuwa huwenda msanii huyo akafunga ndoa.

Subira yavuta heri, cha kuomba uzima ili tarehe hiyo ifike na watu washuhudie ndoa ya staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva iliyosubiriwa na watu wengi kwa hamu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *