Halmashauri zote Mkoani Mtwara zimetakiwa kutenga maeneo kwa ajili ya Michezo na sehemu za kupumzikia,

October 11, 2020

 

Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Mamlaka za Halmashauri zilizopo Mkoani Mtwara zimetakiwa kutenga maneo ya wazi  kwa ajili ya kuendelea michezo na kutengeneza sehemu za kupumzikia.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa wakati wa ufunguzi wa maeneo ya kupumzikia ya Mashujaa (Mashujaa Park) na Tila Park  yaliyopo Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikjindani.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kwa sasa atasimamaia na kuyatunza maeneo ya wazi kwa ajili ya matumizi ya Umma.

‘Nimishapata maombi mara mbili ya kubadilisha matumizi ya eneo la wazi na nikasema walioacha maeneo hayo wanamakusudio yao,kwenye suala la usimamizi wa maeneo ya wazi na michezo mimi nitasimamaia na kuhakikisha yanatunzwa maeneo hayo kwa matmizi ya umma’

Lakini Mkuu wa Mkoa ametoa anngalizo kwa wananchi watakaotembelea maeneo hayo kuhakikisha wanayatunza mazingira ili eneo hilo liweze kuwa endelevu.

Aidha Mkuu wa Mkoa Byakanwa amemsihii Mkurugenzi wa Halmashsuri ya Manispaa Mtwara Mikindani kuhakikisha eneo hilo linawekwa Sheria ndogondogo ili kuendelea kutunza mazingira yake.

‘Tumetengenezezewa eneo zuri hili la kupumzikia , niwasihii wananchi wa Mtwara kuja kwenye maeneo haya ili kupumzika na kushiriki michezo mbali mbali’

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *