Hakuna wakuniweka benchi Yanga – Kaseke

September 17, 2020

 Pamoja na usajili mzuri uliofanywa na Yanga, winga wa timu hiyo, Deus Kaseke, amesema hakuna wa kumweka benchi.Deusi Kaseke anaamini bado ananafasi kwenye kikosi cha Yanga licha ya ingizo la wachezaji wapya kwenye nafasi yakeKaseke ambaye anatajwa kupewa kitambaa cha unahodha anatarajiwa kukutana na upinzania wa namba katika kikosi hicho, baada ya   ujio wa wachezaji wapya Farid Mussa,  Tuisila Kisinda na Juma Mahadhi.Kaseke amesema kwa kipindi  ambacho yupo na Yanga amejifunza mambo mengi yakiwamo ya namna ya kukabiliana na ushindani wa namba.“Kwanza nashukuru wachezaji wanaocheza nafasi yangu kuongezeka kwa sababu kutanipa chachu ya kushindana, lakini pia haitokea  mimi kukaa benchi hapa, ninajiamini naweza kwa asilimia 90. “Kukaa benchi ni suala la mchezaji mwenyewe kukubaliana nalo, lakini kama huhitaji, utatafuta namna ya kufanya mazoezi hata kama ni ya peke yako ili mradi tu ukija mbele ya mwalimu uwe fiti,” amesema.,

 

Pamoja na usajili mzuri uliofanywa na Yanga, winga wa timu hiyo, Deus Kaseke, amesema hakuna wa kumweka benchi.

Deusi Kaseke anaamini bado ananafasi kwenye kikosi cha Yanga licha ya ingizo la wachezaji wapya kwenye nafasi yake

Kaseke ambaye anatajwa kupewa kitambaa cha unahodha anatarajiwa kukutana na upinzania wa namba katika kikosi hicho, baada ya   ujio wa wachezaji wapya Farid Mussa,  Tuisila Kisinda na Juma Mahadhi.

Kaseke amesema kwa kipindi  ambacho yupo na Yanga amejifunza mambo mengi yakiwamo ya namna ya kukabiliana na ushindani wa namba.

“Kwanza nashukuru wachezaji wanaocheza nafasi yangu kuongezeka kwa sababu kutanipa chachu ya kushindana, lakini pia haitokea  mimi kukaa benchi hapa, ninajiamini naweza kwa asilimia 90.

 “Kukaa benchi ni suala la mchezaji mwenyewe kukubaliana nalo, lakini kama huhitaji, utatafuta namna ya kufanya mazoezi hata kama ni ya peke yako ili mradi tu ukija mbele ya mwalimu uwe fiti,” amesema.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *