“Hakuna Urafiki wa Mwanaume na Mwanamke” – Ditto

September 19, 2020

 Msanii wa BongoFleva Lameck Ditto amekataa uwepo wa urafiki wa jinsia mbili tofauti ambao unawahusu mwanaume na mwanamke huku akidai kuwa urafiki wa hivyo lazima uwe na hisia ndani yake au jambo katikati yao. Akifafanua hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio, msanii Ditto amesema kuwa  yeye kama mwanaume anaelewa nini kinakachofuata au kitakachotokea mwisho wa urafiki huo.”Ndani ya urafiki wa mwanaume na mwanamke  lazima kuna Jambo limejificha sijawahi kuona na kama wapo marafiki basi ni mmoja duniani tusidanganyane mimi ni mwanaume naelewa wanaume hatuwezi labda wanawake wanaweza vumilia urafiki ila sisi wanaume hatuwezi” amesema Ditto Aidha Ditto ameendelea kusema “Mwanaume lijali lazima apate hisia hata kama mtakuwa ni marafiki, kuna muda hisia zinakuja asikudanganye mtu urafiki wa jinsia mbili haupo”,

 

Msanii wa BongoFleva Lameck Ditto amekataa uwepo wa urafiki wa jinsia mbili tofauti ambao unawahusu mwanaume na mwanamke huku akidai kuwa urafiki wa hivyo lazima uwe na hisia ndani yake au jambo katikati yao.

 Akifafanua hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio, msanii Ditto amesema kuwa  yeye kama mwanaume anaelewa nini kinakachofuata au kitakachotokea mwisho wa urafiki huo.

“Ndani ya urafiki wa mwanaume na mwanamke  lazima kuna Jambo limejificha sijawahi kuona na kama wapo marafiki basi ni mmoja duniani tusidanganyane mimi ni mwanaume naelewa wanaume hatuwezi labda wanawake wanaweza vumilia urafiki ila sisi wanaume hatuwezi” amesema Ditto 

Aidha Ditto ameendelea kusema “Mwanaume lijali lazima apate hisia hata kama mtakuwa ni marafiki, kuna muda hisia zinakuja asikudanganye mtu urafiki wa jinsia mbili haupo”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *