Hakuna mabadiliko katika mpango wa serikali ya Afghanistan kuwaachia Wataliban, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 3:00 pm

August 29, 2020

Serikali ya Afghanistan imesisitiza kuwa Taliban lazima iwaachie huru makomando waliokamatwa kabla ya kuendelea kuwaachilia huru wafungwa waliobaki wa Taliban kama walivyokubaliana katika mpango wa kuanzisha mazungumzo ya amani.Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama Javad Faisal amesema kwa sasa kuna makomando 22 wa serikali ya Afghanistgan wanaoshikiliwa na Taliban.Masharti hayo yaliwekwa mapema mwezi huu, na Faisal amesema hakuna mabadiliko yoyote katika mpango huo.Kucheleweshwa kuachiwa wafungwa hao katika pande zote ni kizuizi kikuu cha kuanzishwa mazungumzo yaliyosuburiwa ya Waafghanistan ambayo awali yalitarajiwa kuanza Machi 10 chini ya makubaliano kati ya Taliban na Marekani.Serikali ya Afghanistan imewaachia 80 kati ya kundi la wafungwa sugu 400 wa Taliban baada ya kupewa idhini na bunge mnamo Agosti 9.,

Serikali ya Afghanistan imesisitiza kuwa Taliban lazima iwaachie huru makomando waliokamatwa kabla ya kuendelea kuwaachilia huru wafungwa waliobaki wa Taliban kama walivyokubaliana katika mpango wa kuanzisha mazungumzo ya amani.

Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama Javad Faisal amesema kwa sasa kuna makomando 22 wa serikali ya Afghanistgan wanaoshikiliwa na Taliban.

Masharti hayo yaliwekwa mapema mwezi huu, na Faisal amesema hakuna mabadiliko yoyote katika mpango huo.

Kucheleweshwa kuachiwa wafungwa hao katika pande zote ni kizuizi kikuu cha kuanzishwa mazungumzo yaliyosuburiwa ya Waafghanistan ambayo awali yalitarajiwa kuanza Machi 10 chini ya makubaliano kati ya Taliban na Marekani.

Serikali ya Afghanistan imewaachia 80 kati ya kundi la wafungwa sugu 400 wa Taliban baada ya kupewa idhini na bunge mnamo Agosti 9.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *