Habari katika Picha: Harusi ya kitamaduni ya mcheza filamu na mchekeshaji Williams Uchemba na Brunella Oscar

November 17, 2020

Dakika 3 zilizopita

Instagram/williamsuchemba

Mchezaji filamu maarufu wa Nigeria, ambaye kwa sasa amegeuka kuwa mchekeshaji Williams Uchemba amefanya harusi ya kufana ya kitamaduni na mpenzi wake Brunella Oscar mwishoni mwa juma.

Harusi yao ya kufana ilifanyika Alor, Anambra state, ambako ni nyumbani kwa mpenzi wake Brunella

Harusi hii imefanyika wiki kadhaa baada ya kumtaka Williams Uchemba kumuomba uchumba Brunella ambaye alimkubalia na picha za sherehe ya kumvisha pete ya uchumba zilitumwa kwenye mitandao ya kijamii na umma wa wafuasi wake wakawatakia kila la kheri katika safari yao ya mapenzi

Baadaye alifichua kuwa ndoa yao ya kidini itafungwa tarehe 21 Novemba 1, 2020

Mke wa Uchemba ni daktari katika hospitari ya Nigeria inayofahamika kama Hill York Medical.

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram/williamsuchemba

Instagram

Instagram/ten10_drummerboi

Instagram/official_djalonso

Williams Uchemba

Instagram/williamsuchemba

Williams Uchemba ni nani?

Williams Uchemba alianza kazi yake ya filamu akiwa na umri mdogo ambapo alipata umaariufu sana kwa filamu kama ‘Beyond Belief’ na ‘The World of Riches.’

Hivi karibuni alirejea kama mchekeshaji wa mitandao ya kijamii ambapo amepata umaarufu zaidi kwa wimbo wake wenye maneno , “I don’t like what I hate.”

Mwaka 2018, akiwa mchezaji wa filamu, Williams Uchemba alishinda tuzo la mtu binafsi anayehamasisha usaidizi wa jamii na tuzo ya kwanza ya Mitandao ya kijamii.

Uchemba alimekuwa akifanya kampeni ya mitandao ya kijamii inayojulikana kama, ‘Project One Million’ kwa lengo la kuwasaidia watu masikini kupata elimu na ujuzi pamoja na nyumba za garama nafuu.

Mwaka 2018, alikabiliwa na sakata ya ufisadi baada ya mwanaharaka nchini Nigeria, Edafe Okoro kusambaza ujumbe ulioonesha madai ya Uchemba kwamba yeye ni balozi wa Umoja wa Mataifa.

Edafe Okoro alidai kuwa Uchemba alimuomba pesa kwa ajili ya kulipa ili aweze kuwekwa katika ujumbe wa vijana katika tukio la vijana la Umoja wa Mataifa nchini Marekani, akidai kuwa ni balozi wa Umoja wa Mataifa wa vijana.

Kulingana na ushahidi wake aliokuwa ameurekodi katika simu uliosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, Edafe alimfahamisha mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa vijana, Jayathma Wickramanayake na baadaye alitweet akisema kuwa hawakumpata mwakilishi wa Nigeria.

Uchemba alikanusha madai hayo kutoka kwa Edafe pamoja na madai kuwa alijifanya kuwa mjimbe wa Umoja wa Mataifa . Alisema ni kazi ya watu inayolenga kumharibia jina kupitia mitandao ya kijamii.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *