Guterres ataka kusitishwa mapigano Libya,

October 6, 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amezihimiza nchi zenye nguvu duniani na zile zenye maslahi na vita vya muda mrefu vya Libya kuacha kupeleka silaha kwa serikali zinazohasimiana na kuendeleza juhudi za kupatikana kwa mpango wa kudumu wa kusitisha mapigano. 

Matamshi hayo ameyatoa jana wakati wa mkutano wa mawaziri ulioandaliwa kwa ushirikiano wa Ujerumani na Umoja wa Mataifa na kufanyika kwa njia ya video. 

Akizungumza katika mkutano huo wa kuunga mkono juhudi za kupatikana amani ya Libya, Guterres amesema nchi hizo zinapaswa kuonyesha kwa vitendo na sio tu maneno, ikiwemo kuheshimu marufuku ya Umoja wa Mataifa ya kuingiza silaha Libya ambayo inakiukwa. 

Ujerumani imesema mkutano huo ni nafasi ya kupitia upya yale yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele kuhusu Libya uliofanyika Berlin mwezi Januari ambapo wawakilishi kutoka pande zote walikubaliana kuheshimu marufuku ya silaha.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *