Guterres aonya dhuluma dhidi ya wanawake kufuatia janga la corona, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 1, 2020 at 3:00 pm

September 1, 2020

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema janga la COVID-19 limeongeza hali ya kukosekana kwa usawa kati ya wanaume na wanawake na kurudisha nyuma hatua muhimu kuhusiana na masuala ya usawa wa jinsia na haki za wanawake.Guterres aidha amewaonya wasichana waliopo kwenye taasisi za kiraia katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao kwamba iwapo hakutafanyika juhudi za makusudi, kutakuwepo na hatari ya kupoteza hatua iliyopiga katika muda wa kizazi kizima au zaidi.Amesema hii leo mamilioni ya wasichana wadogo kote ulimwenguni hawaendi shule na kuna ripoti zinazotia wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mimba za utotoni katika baadhi ya mataifa.Amezungumzia pia taariza za kukithiri kwa visa vya ghasia dhidi ya wanawake, kwa sababu wanawake hao wanalazimika kukaa na wanyanyasaji wao mahali pamoja tena kwa muda mrefu huku raslimali za kuwasaidia zuikiwa zinaelekezwa kwingineko.,

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema janga la COVID-19 limeongeza hali ya kukosekana kwa usawa kati ya wanaume na wanawake na kurudisha nyuma hatua muhimu kuhusiana na masuala ya usawa wa jinsia na haki za wanawake.

Guterres aidha amewaonya wasichana waliopo kwenye taasisi za kiraia katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao kwamba iwapo hakutafanyika juhudi za makusudi, kutakuwepo na hatari ya kupoteza hatua iliyopiga katika muda wa kizazi kizima au zaidi.

Amesema hii leo mamilioni ya wasichana wadogo kote ulimwenguni hawaendi shule na kuna ripoti zinazotia wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mimba za utotoni katika baadhi ya mataifa.

Amezungumzia pia taariza za kukithiri kwa visa vya ghasia dhidi ya wanawake, kwa sababu wanawake hao wanalazimika kukaa na wanyanyasaji wao mahali pamoja tena kwa muda mrefu huku raslimali za kuwasaidia zuikiwa zinaelekezwa kwingineko.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *