Guterres alaani shambulio dhidi ya raia Nagorno-Karabakh,

October 19, 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitolea wito Armenia na Azabaijan kuheshimu makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na kulaani mashambulio dhidi ya raia wakiwa wanazozania eneo la Nagorno-Karabakh.

 Guterres amelaani hasa shambulio la kombora lilopiga eneo la makazi la mji wa Ganja wa Azerbaijan siku ya Jumamosi, na kuua watu 13 wakiwemo watoto. 

Armenia na Azabaijan zilikubaliana kusitisha mapigani kutoka saa sita usiku, lakini kila mmoja alimlaumu mwenzake kwa kukiuka makubaliano hayo jana Jumapili

 Mapigano hayo yaliyozuka wiki tatu zilizopita ni mabaya zaidi tangu kumalizika kwa vita mnamo mwaka 1994 kati ya nchi hizo mbili. Na yanatishia kuzihusisha nchi kama Uturuki, ambayo inaiunga mkono Azabajani, na Urusi, ambayo ni mshirika wa kijeshi wa Armenia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *