Grealish aongeza mkataba Aston Villa, je ni pigo kwa Man United ?

September 15, 2020

Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 ambaye alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka nane pekee amesaini mkataba huo hii leo ambao utamfanya aendele kusalia Villa kwa miaka mitano zaidi. Na hivyo utamfanya kulipwa mshahara wa paundi 140000 kwa wiki kutoka paundi  70000 alizokuwa akizipata hapo awali.“Ni klabu yangu, hapa ni nyumbani na najisikia furaha hapa.” amesema GrealishGrealish amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktober 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.,

Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 ambaye alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka nane pekee amesaini mkataba huo hii leo ambao utamfanya aendele kusalia Villa kwa miaka mitano zaidi. Na hivyo utamfanya kulipwa mshahara wa paundi 140000 kwa wiki kutoka paundi  70000 alizokuwa akizipata hapo awali.

“Ni klabu yangu, hapa ni nyumbani na najisikia furaha hapa.” amesema Grealish

Grealish amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktober 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *