Giza Nene Jack Patrick, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 29, 2020

DAR: BAADA ya kufungwa miaka 6 jela kwa kosa la kunaswa na madawa ya kulevya nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, swali la “atatoka lini kifungoni?” hakuna alijuaye jibu lake na hivyo kuleta giza nene.Kabrasha za msala wa mrembo huyo zinaonesha kuwa alinaswa kwenye Kisiwa cha Macau nchini China Desemba 19, mwaka 2013 akiwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 1.1. Taarifa halisi zinaonesha kuwa Jack aliingia rasmi kifungoni Agosti 11, 2014 ambapo alitarajiwa kuwa huru Agosti 11, mwaka huu lakini ukimya umetanda hadi sasa.GIZA NENE KUTOKA KWAKE LAZUA HOFU“Hata mimi nashangaa, taarifa zake ni kama zimekatika, zamani nilikuwa nawasiliana naye lakini kwa mwaka huu nimekuwa nikifanya hivyo lakini sijibiwi.“Nini kimemtokea hakuna anayefahamu kwani hata Watanzania walioko China nao ukiwauliza wanasema hawana taarifa zake.“Ni suala la kuendelea kumuombea Mungu, pengine mwezi huu au ujao ataweza kutoka,” alisema rafiki wa karibu na Jack, mkazi wa Mikocheni jijini Dar ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.TAARIFA ZAKE ZASAKWA MITANDAONIKatika hali ambayo ineonesha wengi wanapenda mrembo huyo atoke na kurejea Bongo, mmoja kati ya wadau wake aliposti kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kuuliza: “Jamani mwezi huu si ndiyo Jack Patrik anatakiwa kutoka, hebu mwenye taarifa zake atujuze hapa jamvini.”Hata hivyo, wengi kati ya waliojitokeza kukometi posti hiyo waliishia kumsikitikia, bila kuwepo kwa mtu anayejua nini kinaendelea katika kifungo cha mrembo huyo.MWINGINE ATOA UZOEFU WA KIFUNGOWakati mjadala ukiendelea kuwa hoti mitandaoni, RISASI MCHANGANYIKO lilimtafuta mwanamke mmoja (aliomba asitajwe jina) ambaye amewahi kufungwa China kwa makosa ya kunaswa na madawa ya kulevya na kumuuliza uzoefu wa wafungwa kutoka jela ukoje ambapo alisema:“Hukumu ya Jack haikuwa nzito ilikuwa na wepesi, alikuwa na uwezekano wa kutoka kwa msamaha kama hukumu ilivyosema.“Nafasi ya mfungwa kuingizwa kwenye msamaha hutolewa mara tatu, ukikosa mara ya kwanza utaingizwa kwenye nafasi ya pili, ukikosa hiyo, mara ya tatu ni lazima utoke.“Naamini kama Jack amekosa kutoka kwa mara zote mbili alizokuwa gerezani, basi mwezi wa tisa lazima atatoka. “Tuendelee kumuombea amalize salama kifungo chake na arudi nyumbani tuendelee kulijenga taifa letu.”TUJIKUMBUSHEJack Patrick alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.Akitumia dakika 27, kusoma hukumu, Hakimu kwenye mahakama moja nchini humo alimtia hatiani Jack kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani.Jack kabla ya kufikwa na janga hilo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii maarufu Juma Khalid ‘Jux’ ambaye anatajwa kumtungia wimbo mpenzi wake huyo aliupa jina la Nitasubiri akimaanisha atamsubiri Jack atoke gerezani waendelee na yao.stori Mwandishi Wetu, Risasi,

DAR: BAADA ya kufungwa miaka 6 jela kwa kosa la kunaswa na madawa ya kulevya nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, swali la “atatoka lini kifungoni?” hakuna alijuaye jibu lake na hivyo kuleta giza nene.

Kabrasha za msala wa mrembo huyo zinaonesha kuwa alinaswa kwenye Kisiwa cha Macau nchini China Desemba 19, mwaka 2013 akiwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 1.1. Taarifa halisi zinaonesha kuwa Jack aliingia rasmi kifungoni Agosti 11, 2014 ambapo alitarajiwa kuwa huru Agosti 11, mwaka huu lakini ukimya umetanda hadi sasa.

GIZA NENE KUTOKA KWAKE LAZUA HOFU

“Hata mimi nashangaa, taarifa zake ni kama zimekatika, zamani nilikuwa nawasiliana naye lakini kwa mwaka huu nimekuwa nikifanya hivyo lakini sijibiwi.

“Nini kimemtokea hakuna anayefahamu kwani hata Watanzania walioko China nao ukiwauliza wanasema hawana taarifa zake.

“Ni suala la kuendelea kumuombea Mungu, pengine mwezi huu au ujao ataweza kutoka,” alisema rafiki wa karibu na Jack, mkazi wa Mikocheni jijini Dar ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.

TAARIFA ZAKE ZASAKWA MITANDAONI

Katika hali ambayo ineonesha wengi wanapenda mrembo huyo atoke na kurejea Bongo, mmoja kati ya wadau wake aliposti kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kuuliza: “Jamani mwezi huu si ndiyo Jack Patrik anatakiwa kutoka, hebu mwenye taarifa zake atujuze hapa jamvini.”

Hata hivyo, wengi kati ya waliojitokeza kukometi posti hiyo waliishia kumsikitikia, bila kuwepo kwa mtu anayejua nini kinaendelea katika kifungo cha mrembo huyo.

MWINGINE ATOA UZOEFU WA KIFUNGO

Wakati mjadala ukiendelea kuwa hoti mitandaoni, RISASI MCHANGANYIKO lilimtafuta mwanamke mmoja (aliomba asitajwe jina) ambaye amewahi kufungwa China kwa makosa ya kunaswa na madawa ya kulevya na kumuuliza uzoefu wa wafungwa kutoka jela ukoje ambapo alisema:

“Hukumu ya Jack haikuwa nzito ilikuwa na wepesi, alikuwa na uwezekano wa kutoka kwa msamaha kama hukumu ilivyosema.

“Nafasi ya mfungwa kuingizwa kwenye msamaha hutolewa mara tatu, ukikosa mara ya kwanza utaingizwa kwenye nafasi ya pili, ukikosa hiyo, mara ya tatu ni lazima utoke.

“Naamini kama Jack amekosa kutoka kwa mara zote mbili alizokuwa gerezani, basi mwezi wa tisa lazima atatoka. “Tuendelee kumuombea amalize salama kifungo chake na arudi nyumbani tuendelee kulijenga taifa letu.”

TUJIKUMBUSHE

Jack Patrick alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

Akitumia dakika 27, kusoma hukumu, Hakimu kwenye mahakama moja nchini humo alimtia hatiani Jack kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani.

Jack kabla ya kufikwa na janga hilo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii maarufu Juma Khalid ‘Jux’ ambaye anatajwa kumtungia wimbo mpenzi wake huyo aliupa jina la Nitasubiri akimaanisha atamsubiri Jack atoke gerezani waendelee na yao.

stori Mwandishi Wetu, Risasi,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *