Ghani aitaka Taliban kuweka chini silaha,

October 7, 2020

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani amelitaka kundi la Taliban kuwa na ujasiri na kuweka chini silaha. Wito huo ameutoa jana wakati alipoizuru Doha, ambako mazungumzo ya amani kati ya wapatanishi wa serikali na Taliban yamekwama. 

Mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili na ya kwanza Doha tangu kuanza kwa mazungumzo, Ghani alisema mzozo wa muda mrefu unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na sio kwa mtutu wa bunduki. 

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanayosimamiwa na Qatar, yana lengo la kuvimaliza vita vya Afghanistan vilivyodumu kwa miaka 19. 

Hata hivyo, mazungumzo hayo yanasuasua kutokana na kutokubaliana jinsi ya kuweka kanuni za maadili ambazo zitayaongoza mazungumzo hayo.

 Masuala kadhaa ikiwemo kusitisha mapigano au muundo wa serikali ambao utazungumzia mustakabali wa Afghanistan, bado hayajajadiliwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *