Genge la watu wenye mapanga lawashambulia waandamanaji Nigeria,

October 15, 2020

Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamekuwa yakiendelea katika miji mikubwa kote NigeriaImage caption: Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamekuwa yakiendelea katika miji mikubwa kote Nigeria

Waandamanaji dhidi ya ghasia za polisi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja wameshambuliwa na wanaume wasiojulikana waliokuwa wamebeba mapanga.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema mamia ya waandamanaji kadhaa walikuwa wamekusanyika katika kati ya mji huo wakati shambulio lilipotokea.

Muandamanaji mmoja amesema baadae baadhi ya wavamizi hao walikamatwa na kukabidhiwa kwa maafisa.

Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji mbalimbali kote nchini Nigeria kwa wiki nzima iliyopita. Ghasia zimeendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi- cha kukabiliana na wizi kinachofahamika kama Sars.

Waandamanaji wameapa kuendelea kuwepo mitaani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *