Gari Yaacha Njia, Yapinduka Na Kusababisha Majeruhi Na Uharibifu Wa Mali Jijini Mbeya, on September 10, 2020 at 10:00 am

September 10, 2020

Mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 06:40 Asubuhi huko maeneo ya Inyala – Mablock, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Njombe, Gari lenye namba ya usajili T.629 CQC Scania Basi mali ya Kampuni ya ISAMILO EXPRESS likitokea Mbeya kwenda Mwanza likiendeshwa na Dereva aitwaye KINI DAUD MALIMI [51] Mkazi wa Igoma Mwanza liliacha njia, kupinduka na kusababisha majeruhi na uharibifu wa Gari hilo na baadhi ya mali za abiria.Katika ajali hiyo abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake ambapo majeruhi 08 kati yao wanaume 05 na wanawake 03 wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine 14 kati yao 07 ni wanaume na 07 ni wanawake wanaendelea kupatiwa matibabu Kituo cha Afya Inyala.Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari pamoja na mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali.Imetolewa na:[ULRICH MATEI – SACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.,

Mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 06:40 Asubuhi huko maeneo ya Inyala – Mablock, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Njombe, Gari lenye namba ya usajili T.629 CQC Scania Basi mali ya Kampuni ya ISAMILO EXPRESS likitokea Mbeya kwenda Mwanza likiendeshwa na Dereva aitwaye KINI DAUD MALIMI [51] Mkazi wa Igoma Mwanza liliacha njia, kupinduka na kusababisha majeruhi na uharibifu wa Gari hilo na baadhi ya mali za abiria.


Katika ajali hiyo abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake ambapo majeruhi 08 kati yao wanaume 05 na wanawake 03 wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine 14 kati yao 07 ni wanaume na 07 ni wanawake wanaendelea kupatiwa matibabu Kituo cha Afya Inyala.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari pamoja na mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali.

Imetolewa na:
[ULRICH MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *