Fulham Wajitosa Kumbakisha Samatta England

September 20, 2020

KLABU ya Fulham inayoshiriki Ligi Kuu England ‘Premier’ imeingia katika vita ya kumsajili mshambuliaji, Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Aston Villa.Hiyo ni baada ya Fenerbahce ya Uturuki na West Brom ya England kuanza kumuwinda.West Brom wapo tayari kumchukua kwa mkopo au kumnunua moja kwa moja, huku Fenerbahce ikimtaka kama mbadala wa Vedat Muriqi aliyeuzwa Lazio ya Italia.Aston Villa ipo tayari kumuachia mchezaji huyo aliyetua kikosini hapo Januari, mwaka huu kwa dau la pauni mil 10 akitokea KRC Genk.Akizungumza na Spoti Xtra, baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Mzee Ally Samatta, alisema: “Nimeongea naye usiku wa jana (juzi) baada ya kusoma taarifa kwamba ameenda Uturuki, akaniambia bado yupo England.“Mwenyewe anasema yupo njia panda licha ya kutakiwa na timu nyingi kama Fenerbahce, Galatasary na Besiktas za Uturuki, na hapo England wameongezeka Fulham.Nimeshamwambia abaki England japo ana uamuzi wake.”Samatta hivi sasa ameonekana ana nafasi finyu ya kucheza baada ya Aston Villa kusajili washambuliaji wawili ambao ni Ollie Watkins na Bertrand Traore.,

KLABU ya Fulham inayoshiriki Ligi Kuu England ‘Premier’ imeingia katika vita ya kumsajili mshambuliaji, Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Aston Villa.

Hiyo ni baada ya Fenerbahce ya Uturuki na West Brom ya England kuanza kumuwinda.West Brom wapo tayari kumchukua kwa mkopo au kumnunua moja kwa moja, huku Fenerbahce ikimtaka kama mbadala wa Vedat Muriqi aliyeuzwa Lazio ya Italia.

Aston Villa ipo tayari kumuachia mchezaji huyo aliyetua kikosini hapo Januari, mwaka huu kwa dau la pauni mil 10 akitokea KRC Genk.

Akizungumza na Spoti Xtra, baba mzazi wa mshambuliaji huyo, Mzee Ally Samatta, alisema: “Nimeongea naye usiku wa jana (juzi) baada ya kusoma taarifa kwamba ameenda Uturuki, akaniambia bado yupo England.

“Mwenyewe anasema yupo njia panda licha ya kutakiwa na timu nyingi kama Fenerbahce, Galatasary na Besiktas za Uturuki, na hapo England wameongezeka Fulham.

Nimeshamwambia abaki England japo ana uamuzi wake.”Samatta hivi sasa ameonekana ana nafasi finyu ya kucheza baada ya Aston Villa kusajili washambuliaji wawili ambao ni Ollie Watkins na Bertrand Traore.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *