Fisi Aliyeua Mtoto, Kujeruhi Wawili Auawa

October 5, 2020

 

FISI aliyeua mtoto na kujeruhi watu wazima wawili jana, Septemba 4, 2020,  mchana katika Kijiji cha Mbogo, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu,  ameuawa na askari wa kikosi cha ujangili cha Maswa na Bunda.

Fisi huyo anayesemekana alitoka katika pori la akiba la Maswa alimvamia na kumuua mtoto  wa kike, Kwangu Makanda (11) ambapo waliojeruhiwa Fatili Lindai Tungu ($#) na Miranda Sali Nyamoko Mwanaume (55) ambao walipelekwa hospitali ya wilayani Ikindilo kwa  matibabu.

Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) umekuwa ukifanya jitihada kubwa mkoani humo kudhibiti wanyama hatari kwa ajili ya kuokoa maisha ya binadamu au kuzuia madhara ambayo yangeweza kusababishwa na wanyama hao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *