Filamu ya wapenzi wa jinsia moja yazua mjadala mkali Nigeria

September 15, 2020

Dakika 5 zilizopita

Photo cover of Ife showing two women facing each other

Watayarishaji filamu wawili nchini Nigeria wanakabiliwa na tisho la kufungwa ikiwa watapuuza onyo kali walilopewa na bodi ya filamu nchini humo na kuendelea mbele na mpango wa kuachia filamu inayohusu wapenzi wa jinsia moja.

Mtayarishaji wa filamu hiyo Pamela Adie na muongozaji wake Uyaiedu Ikpe-Etim wanashikilia kuwa Ife (kumaanisha”mapenzi” kwa lugha ya Kiyoruba ) inawaangazia Wanigeria, lakini bodi ya filamu NFVCB inasema haitaidhinisha kwasababu inakiuka maadili ya nchi na sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Kuoneshwa kimataifa

Ili kukabiliana na kizingiti hicho waandaji filamu hao wanapanga kuiachilia mitandaoni. Bodi ya NFVCB, hata hivyo, inafuatilia kwa makini mitandao yote ya kijamii kuzuia filamu hiyo isiwafikie walengwa.

Kwa mujibu wa mkuu wa NFVCB Adebayo Thomas, Adie na Ikpe-Etim huenda wakafungwa jela kwa ku tukuza usagaji katika nchi ambayo mapenzi ya jinsia moja yamepigwa marufuku na huenda wakafungwa jela hadi miaka 14.

Wanapanga onyesho la faragha la filamu hiyo katika mji wa kibiashara wa Lagos, mwisho wa mwezi huu, katika hatua ambayo wanaamini hawahitaji kutafuta ruhusa ya kufanya hivyo. Ife pia itaonyeshwa katika hafla ya kimataifa nchini Canada mwezi Oktoba.

Pamela Adie quote

Adie anasema lengo la filamu hiyo ni kutoa mtazamo halisi kuhusu wanawake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja tofauti na wanawake wengine katika filamu za Nigeria.

Ikiwa mwanamke msagaji anaonekana kwenye sinema ya kawaida ya Nollywood mara nyingi huonyeshwa kuwa amepagawa, kushawishiwa na marafiki wabaya au kulazimishwa kufanya mapenzi ya jinsia moja na kila wakati anahitaji “kuokolewa”, aliambia BBC.

“Ni nadra sana kuona filamu zinavyoangazia wapenzi wa jinsia moja, hususan kuhusu wanawake wanaozungumzia uhalisia wa maisha yetu.

“Ife imeandaliwa kuziba pengo hilo na kuibua mjadala huo nchini Nigeria.”

Kutoka kwa mama wa Nigeria

Ife ni hadithi ya wanawake wawili ambao walipendana baada ya kuwa pamoja kwa siku tatu. Baadae “mapenzi yao yanakabiliwa na mtihani mgumu kutokana na uhalisia wa maisha kuhusu wapenzi wa jinsia moja katika nchi kama Nigeria”, kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa kwa umma kuhusu filamu hiyo.

Tukizingatia tangazo la awali lililooneshwa Julai ambapo ngono iliashiriwa lakini haikuoneshwa, basi Ife imevuka mipaka ya kuelezea hadithi ya wapenzi wa jinsia moja kulingana na kanuni zinaoongoza uandaji wa filamu nchini Nigeria.

Uzoamaka Aniunoh (Kushoto) na Cindy Amadi (Kulia)

Maelezo ya picha,

Uzoamaka Aniunoh (Kushoto) na Cindy Amadi (Kulia), wanaonekana hapa, wakiifiza filamu ya wapenzi wawili wa kike

Katika mojawapo ya sehemu ya filamu hiyo washirika wakuu, Ife na Adaora wanazunguzia mapenzi na changamoto zinazowakabili watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja huswa ndani ya familia yao.

Mazungumzo hayo yalitumiwa kuonadi filamu hiyo.

“Nilimwambia mama kwanza, ilimchukua wiki nzima kutafakari kile nilichomwambia,” Mhusika Ife, ambayo imeigizwa na Uzoamaka Aniunoh, anasema alikuwa akizungumzia utambulisho wake kwamba ni msagaji.

“Ambayo kwa ufupi inamaanisha mama wa Kinigeria,” mhusika wa pili ni Adaora, ambayo imeigizwa na Cindy Amadi.

“Ni mapema sana kusema huenda unanipenda?” anauliza Adaora huku wakipapasana.

“Sisi ni wasagaji, na huu ndio muda mwafaka,” anajibu Ife.

Inahitaji kufanyiwa maboresho

Mapenzi ya jinsia moja ni suala tata sana katika nchi nyingi barani Afrika na Nigeria sio tofauti.

Nigeria ni jamii ya watu wa waliokumbatia dini na utamaduni kutokana na ushawishi wa imani ya Kikristo na Kiislamu dini ambazo zinapinga mapenzi ya jinsia moja.

Sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia ilipitishwa mwaka 2014 na ilitungwa enzi ya ukoloni kuzuia ulawiti. Polisi wamefanya msako wa kuwakamata watu wanaosuhukiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja hatua iliyowafanya baadhi yao kukimbilia mafichoni.

Ikpe-Etim quote

Hisia ya kutengwa na hitaji la kupinga imani kwamba ushoga ni uasherati ndio ilimhimiza mkurugenzi Ikpe-Etim kuchukua mradi huo.

“Kabla ya sasa, tulisimuliwa hadithi zinazoegemea upande mmoja. Tunachofanya na filamu hii ni kusawazisha masuala hayo, na kufanya mapenzi ya jinsia moja kuwa jambola kawaida” aliiambia BBC.

Jamii ya wapenzi wa jinsia moja barani Afrika wamekuwa wakishinikiza jamii kuwatambua na kuwakubali na wamekuwa wakitumia fursa za intaneti kurusha filamu na vipindi vyao mitandaoni.

Presentational grey line

Hata hivyo mpango huo haujawakinga watayarishaji filamu kujipata mashakani.

Mkuu wa NFVCB alisema hakuna nafasi ya Ife au sinema zingine za ushoga nchini Nigeria, akizingatia sheria.

“Kuna sheri ainayopinga mapenzi ya jinsia moja, iwe ni kwa maisha ya kawaida au kuigiza kwenye filamu. Ikiwa maudhui ni ya kutoka Nigeria, lazima ichunguzwa,” Bw Thomas aliiambia BBC.

Alisema kuwa jukwaa lolote litakalotumiwa, “alimradi maudhui yanaangazia Nigeria na inasimulia hadithi ya Nigeria, basi inatuhusu”

A man stands in a shop selling Nollywood films

Maelezo ya picha,

Ife sio filamu ya kawaida ya Nigeria inayojulikana kwa jina maarufu Nollywood

Mwitikio wa filamu za wapenzi wa jinsia moja ukoje Afrika

Hii sio mara ya kwanza filamu zilizo na maudhui ya wapenzi wa jinsia moja zimejipata mashakani na malaka zinazodhibiti maudhui barani Afrika

Filamu ya ”Hadithi za maisha yetu”, ambayo ni mkusanyiko wa filamu tano fupi zilizoangazia maisha ya wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya ilipigwa marufuku mwaka 2014 kwa “kuenda kinyume na maadili ya kitaifa”.

Pia kuna filamu ya Rafiki, ambayo ilikuwa ya kwanza kuangazia uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Filamu hiyo ilioneshwa katika tamasha la filamu la Cannes na pia iliteuliwa katika tuzo za Oscar.

Inxeba/The Wound, Filamu kutoka Afrika Kusini iliangazia uhusiano wa wanaume wawili katika muktadha wa matambiko ya Xhona pia ilipigwa marufuku kuoneshwa kwenye kumbi za sinema 2018.

Licha ya changamoto zinazowakabili wapenzi wa jinsia moja barani Afrika wanasema wamepata ujasiri na wanaimani siku moja watakubalika katika jamiii na kuonekana zaidi kwenye filamu na fasihi ambayo inahimiza kuvumiliana.

Source link

,Dakika 5 zilizopita Chanzo cha picha, PAmela Adie Watayarishaji filamu wawili nchini Nigeria wanakabiliwa na tisho la kufungwa ikiwa watapuuza…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *