Felicien Kabuga: UN yawateuawa majaji watatu watakaosimamia kesi ya mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda

October 2, 2020

Dakika 3 zilizopita

Majaji watatu walioteuliwa kusimamia kesi ya kabuga

Maelezo ya picha,

Majaji watatu walioteuliwa kusimamia kesi ya kabuga

Mahakama ya Umoja wa mataifa imewateua majaji watatu watakaosimamia kesi inayomkabili Felicien Kabuga.

Kamati ya Umoja mataifa kuhusu mahakama za uhalifu imewateua majaji hao kutoka mataifa ya Uskochi, Uruguay na Uganda kusimamia kesi ya Kabuga atakapowasilishwa katika mahakama ya Tanzania kujibu mashtaka ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Siku ya Jumatano mahakama ya Ufaransa iliunga mkono kushtakiwa kwake katika mahakama ya Umoja wa mataifa iliopo Arusha.

Wakili wake Emmanuel Altit aliambia BBC kwamba atakwenda katika kaati hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kesi za uhalifu ili kuhakikisha kwamba anahamishwa hadi mjini The Hague, Uholanzi ambapo kamati hiyo ina tawi lake.

Sheria za uhamisho za Ufaransa zinatoa mwezi mmoja kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Katika taarifa yake, Mahakama hiyo ya Arusha haikusema ni wakati gani kesi inayomkabili Kabuga itaanza.

Jaji wa Uskochi Lain Bonomy, ataongoza usimamizi wa kesi hiyo akisaidiwa na majaji wa Uruguay Graciela Susana Gatti Santana na jaji wa Uganda Elizabeth Ibanda – Nahamya, ilisema mahakama hiyo ya UN.

Bwana Kabuga mwenye umri wa miaka 85, ndio mtu maarufu kuwahi kushtakiwa na mahakama hiyo ya kimataifa 1997, ilisema mahakama hiyo , lakini alienda mafichoni hadi alipokamatwa karibu na mji wa Paris mnamo mwezi Mei 2020.

Katika mahakama ya Paris ameelezea mashtaka yanayomkabili kama ya uwongo.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *