Fahamu desturi ya wanaanga wa Urusi ya kujikojolea kabla ya kuanza safari

October 18, 2020

Dakika 5 zilizopita

Yuri Gagarin, 1961, justo antes del despegue.

Maelezo ya picha,

Yuri Gagarin aliweka historia mwaka 1961. Picha hii ilichukuliwa dakika chache kabla ya kuanza safari.

Alikuwa kwenye barabara kuu kusini mwa Kazakhstan, akielekea kwenye kituo cha anga cha Baikonur Cosmodrome, kituo cha anga cha kale na kikubwa zaidi duniani. Ghafla akataka kujisaidia tena kwa haraka.

Akiwa amebanwa na mikojo, mwanaanga huyo, 27, alimuomba dereva wa basi kuegesha gari kidogo. Alitoka nje na kufungua sehemu fulani ya nguo rasmi ya kwenda anga za mbali ambayo tayari alikuwa ameshavaa akajisaidia haja ndogo.

Kipindi hicho akiwa anakaribia kuweka historia… kuwa mwanadamu wa kwanza kwenda kwenye anga za mbali! Lakini kibofu chake kikashindwa kuzuia mikojo.

Na tangu wakati huo, Aprili 12, 1961, wanaanga wote wanaokwenda anga za mbali wamekuwa wakijisaidia muda kidogo tu kabla ya kuanza safari kama ilivyokuwa kwa Gagarin.

Kwa wengi ni kama desturi au utamaduni ambao ni lazima ufanywe.

Wengine wanafanya kama vile ushirikina au waepuke kutofanya kule kukosa kuitekeleza. Lakini wanaanga huakikisha wanaitimiza hata kwa wanawake pia ambao mara nyingi hubeba mikojo na kuimwaga kidogo kwenye vazi rasmi la kwenda katika anga la mbali.

Cosmonautas rusos

Maelezo ya picha,

Kurudia kilichofanywa na Gagarin yaani kukojoa kabla ya kuanza safari ni utamaduni ambao umekuwa ukitekelezwa na wanaanga wengi.

“Lazima nikojoe”

Historia ya Gagarin inaweza kuonekana kama aibu lakini ni wazi kwamba unaposhikwa ni mikojo haswa, inakuwa vigumu sana kuizuia. Angalau yeye alizuia kujikojolea kama ilivyotokea kwa Alan Sherpard, Mmarekani wa kwanza kusafiri kwenye anga la mbali Mei 5 mwaka huo huo.

Ilitakiwa kuwa safari ya muda mfupi, takriban dakika 15 tu, lakini ikachelewa kuanzishwa na timu hiyo haikuwa imezingatia mkojo kama jambo la dharura linaloweza kutokea.

“Lazima nikojoe,” Shepard mara moja akawaarifu wadhibiti kabla ya chomboo kupaa. Wakati huo alikuwa amekisubiri kwa saa tatu na hakuweza tena kuvumia. Unajua jibu alilopata lilikuwa gani? ”jikojolee kwasababu hatuna tena muda”.

Na yeye naye akawa hana budi zaidi ya kufanya hivyo: Aliketi taratibu tena bila hata kujisongeza songeza bila shaka hakuwa huru huku kamera zikinasa wakati huo wa kihistoria.

Wahandisi walikuwa na wasiwasi. Je itakuwaje ikiwa mikojo itagusa nyaya iliyopo kwenye vazi hilo maalum? Lakini bahati nzuri haikufika huko.

“Vazi hilo ambalo kitambaa chake kilikuwa ni pamba papo hapo ilinyonya mikojo,” kulingana na rekodi za Shirika la Kituo cha Anga za Mbali (NASA) kuhusu alichosema Shepard kwa tukio hilo. “[Nguo yake] ilikuwa imekauka kufikia wakati wa kuanza kwa safari yake.”

Alan Shepard, 5 de mayo de 1961, antes del lanzamiento.

Maelezo ya picha,

Picha ya Shepard inayoonesha uso wake muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa safari inajieleza yenyewe

Tukio hilo likawa chanzo cha Shirika la NASA kuunda nguo za kwenda kwenye anga la mbali zenye mfumo maalum na vifaa vingine kama vile mifuko, ili wanaanga waweze kuwa na sehemu ya kujisaidia. Baadae, vyombo vya kusafiria vikawekwa vyoo.

Ilustración de la primera caminata espacial rusa

Maelezo ya picha,

Así son los Sokol-KV2 que los astronautas rusos usan actualmente, desde los años 80.

Siku hizi, wanaanga huvaa nepi inayonyonya mikojo – ambazo zinawawezesha kutokuwa na ulazima wa kwenda chooni kwa saa kipindi kirefu mfano wake ni vile unavyomvalisha mtoto nepi usiku kama analala.

Takriban asilimia 80 hadi 85 ya mkojo huchakatwa tena kutengenezwa maji ya kunywa kwa wanaanga.

Hata hivyo, wanaanga wa Urusi bado mpaka sasa hutumia vazi lao la tangu kale linalowawezesha kwenda haja ndogo humo humo.

Vazi jipya lenye kuzua utata

Yuri Gagarin, 1961, minutos antes del lanzamiento

Maelezo ya picha,

Nguo aliyovaa Gagarin katika safari yake ya kwanza kwenda anga la mbali ilimwezesha kukojoa akiwa amesimama lakini muundo wa vazi jipya ni tofauti.

Swali ni je, desturi ya wanaanga kukojoa kwenye vazi lao kabla ya safari kuanza utamaduni ambao chimbuko lake ni mwanaanga wa kwanza je kutalazimisha kubadilishwa kwa vazi hilo la Urusi ambalo bado halijatangazwa linatolewa lini rasmi.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Christina Koch: Mwanamke aliyeishi kwenye anga za mbali kwa muda mrefu

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *