EURO 2020: Mambo Matano muhimu kuhusu michuano hiyo

June 11, 2021

Dakika 6 zilizopita

euro

Chanzo cha picha, Reuters

Ilikuwa mwaka, miezi na sasa zinahesabika dakika kabla ya kuanza kwa Mashindano ya Euro 2020 Juni 11 mpaka Julai 11 mwaka huu. Mashindano haya yalikuwa yafanyike Juni 12 mpaka Julai 12 mwaka jana lakini yaliahirishwa kwa sababu ya uwepo wa janga la Corona.

Jumla ya timu 24 zitashiriki mashindano hayo katika mechi 51 zitakazopigwa katika majiji 11 ya nchi za Ulaya, hata hivyo haifahamika ni kiasi gani cha mashabiki wataruhusiwa kuingia viwanjani kushuhudia michuano hiyo, kutokana na janga la Corona kuendelea katika maeneo mbalimbali ya bara hilo. Kwa mara ya kwanza pia michuano yam waka huu itatumia usaidizi wa video kwenye maamuzi (VAR).

1: Kundi gumu zaidi ‘kundi la Kifo’

Yapo makundi sita ya timu nne ne kila kitu, ambapo kundi gumu zaidi linatajwa kuwa ni kundi F linalojumuisha timu za Ujerumani, Ufaransa, Ureno na Hungary. Ukiacha Hungary, mechi baina ya timu zingine tatu za kundi hilo ni ngumu kutabirika huku zikiwa na vikosi vyenye nyota wengi wanaocheza vilabu vikubwa Ulaya.

Ufaransa ni bingwa wa sasa wa kombe la dunia, Ureno ni mabingwa watetezi wa mashindano hayo na Ujeruani ni mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2014. Ujerumani watacheza mechi zake tatu za hatua ya makundi mjini Munich, huku mechi zingine za kundi hilo zikifanyika mjini Budapest.

“Hili ni kundi la kifo,” alisema kocha wa Ujerumani Joachim Low, ambaye atang’atuka baada ya michuano hiyo.

Haya ni mashindano ya pili ambapo bingwa wa kombe la dunia anakutana na bingwa wa Ulaya kwneye hatua za makundi, ilikuwa hivyo katika michuano ya Euro 1992, Uholanzi ilipokutana na Ujerumani.

Group A: Italy, Switzerland, Turkey, Wales

Group B: Belgium, Russia, Denmark, Finland

Group C: Ukraine, Netherlands, Austria, North Macedonia

Group D: England, Croatia, Czech Republic, Scotland

Group E: Spain, Poland, Sweden, Slovakia

Group F: Germany, France, Portugal, Hungary

2: Kwa nini mashindano ya mwaka huu yanachezwa kwenye miji 11?

Mwaka huu, UEFA inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo. Kabla ya janga la corona , mashindano haya yalipangwa kufanyika mwaka jana huko Rome, Italia, lakini janga la Corona likayasimamisha mashindano hayo. Kuhairishwa kwa mashindano hayo kutoka mwaka 2020 kuja 2021, ikatoa fursa ya Kamati ya utendaji ya UEFA ikaamua kuyapelekea mashindano hayo kwenye majiji 11 ya nchi za Ulaya ili yawe wenyeji ya michuano hiyo kama sehemu ya kuadhiisha miaka hiyo 60 ya michuano ya Euro.

Majiji hayo 11 ni Amsterdam, Baku, Bucharest, Budapest, Copenhagen, Glasgow, Munich, London, Rome, Seville na St Petersburg. Awali majiji ya Dublin na Bilbao yalipangwa kuwa sehemu ya wenyeji lakini yaliondolewa baada ya kushindwa kufikia vigezo, na kuongezwa jiji la Seville.

Gary Lineker, Gabby Logan, Eilidh Barbour and Mark Chapman will lead coverage across TV and radio and will be joined by a host of former England, Scotland and Wales stars

Uwanja wa Wembley katika jiji la London wenye uwezo wa kubeba watazamaji 90,000 ndio utakaotumika kwenye mchezo wa fainali , nusu fainali zote mbili, mechi mbili za hatua ya 16 bora na mechi tatu za makundi. Uwanja wa Hampden Park, uliopo katika jiji la Glasgow, Scotland wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 51,000, utakuwa mwenyeji wa mechi tatu za makundi na moja ya hatua ya 16 bora.

Viwanja vingine vitakavyotumika ni Estadio de La Cartuja, uliopo Seville, Johan Cruyff Arena (Amsterdam), Stadio Olimpico (Rome), viwanja vingine ni Puskas (Budapest), Krestovsky Stadium, (St Petersburg), Arena Nationala, (Bucharest), Parken Stadium (Copenhagen), Football Arena Munich (Munich) na Olympic Stadium (Baku).

3: Wachezaji 624 kushiriki Michuano ya Euro mwaka huu.

Michuano ya mwaka huu, kila timu imeruhusiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyokuwa huko nyuma. Idadi hiyo imeongezwa kwa sababu ya kutoa unafuu kwasababu ya janga la corona, idadi inayofanya mashindano hayo kushirikisha jumla ya wachezaji 624.

Pamoja na kuruhusiwa kuwa na wachezaji 26, ni wachezaji 23 tu watakaruhusiwa kuwa katika orodha ya kutumika kwa ajili ya mechi za mashindano hayo.

4: Dola milioni 452 kutolewa kama zawadi mwaka huu

Jumla ya zawadi zote zitakazotolewa mwaka huu kwenye mashindano hayo ni dola milioni 452 million. Zawadi hii ya fedha ni kubwa zaidi kuliko zawadi zilizotolewa katika mashindano yaliyopita ya Euro 2016 nchini Ufaransa. Kila nchi shiriki inatarajiwa kupokea kitita cha dola milioni 11.2, huku mshindi akijizolea dola milioni 41.4.

5: Je mashabiki wataruhusiwa kuingia viwanjani?

Kwa mujibu wa UEFA, kila kiwanja kitakachotumika kitaruhusiwa kuingiza mashabiki kadhaa kwa vigezo vilivyokubalika ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Viwanja vya St Petersburg na Baku vimethibitisha kuingiza asilimia 50% ya uwezo wa viwanja hivyo, huku Puskas ulioko Budapest ikitatazamia kuruhusu asilimia 100% ya uwezo wa uwanja huo.

Viwanja katika majiji ya Amsterdam, Bucharest, Copenhagen, Glasgow, Rome na Seville wao wataruhusu mpaka robo ya uwezo wa viwanja vyao.

Uwanja wa Wembley ambao utachezwa mechi ya fainali, umethibitisha kuruhusu robo tu ya wa mashabiki katika mechi tatu za hatua ya makundi kama ilivyo kwa Football Arena Munich, ulioko Munich.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *