EU yayumba kuichukulia Urusi hatua kuhusu Navalny, on September 8, 2020 at 10:00 am

September 8, 2020

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yametishia kuiwekea vikwazo Urusi kuhusiana na shambulio la sumu inayoathiri mishipa ya fahamu dhidi ya kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lakini uamuzi wa pamoja utakuwa mgumu kufikiwa kutokana na maslahi yaliyopo. Mataifa ya mataifa ya magharibi yanaungana katika kukasirishwa na majaribio kadhaa ya mauaji dhidi ya wakosoaji wa rais Vladimir Putin. Na katika suala la Navalny pia kuna wasi wasi mahsusi wakati madaktari wa Ujerumani wanasema kulikuwa na matumizi ya sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok. Umoja wa Ulaya wiki iliyopita ulilaani matumizi ya silaha za sumu kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kuionya Urusi kuwa itachukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na vikwazo. Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa jibu la kimataifa linahitajika lakini amekataa kutabiri kuhusu aina ya htua zitakazochukuliwa.,

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yametishia kuiwekea vikwazo Urusi kuhusiana na shambulio la sumu inayoathiri mishipa ya fahamu dhidi ya kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lakini uamuzi wa pamoja utakuwa mgumu kufikiwa kutokana na maslahi yaliyopo. 

Mataifa ya mataifa ya magharibi yanaungana katika kukasirishwa na majaribio kadhaa ya mauaji dhidi ya wakosoaji wa rais Vladimir Putin. 

Na katika suala la Navalny pia kuna wasi wasi mahsusi wakati madaktari wa Ujerumani wanasema kulikuwa na matumizi ya sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok. 

Umoja wa Ulaya wiki iliyopita ulilaani matumizi ya silaha za sumu kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kuionya Urusi kuwa itachukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na vikwazo. 

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa jibu la kimataifa linahitajika lakini amekataa kutabiri kuhusu aina ya htua zitakazochukuliwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *