EU yatafakari kuchukua vikwazo dhidi ya Uturuki kuhusu mzozo wa Mediterania, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 3:00 pm

August 29, 2020

Umoja wa UIaya unatafakari kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Uturuki kwa sababu ya utafiti wake wa gesi mashariki ya Bahari ya Mediterania, eneo ambalo linagombaniwa na Ugiriki.Akizungumza baada ya mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya mjini Berlin, Mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borell amesema kutokana na kukosekana kwa maendeleo katika suala hilo, huenda wakatayarisha orodha ya vikwazo zaidi.Baadae suala hilo litajadiliwa katika mkutano ujao wa kilele Septemba 24. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema kuupanua wigo wa vikwazo dhidi ya Uturuki kutahitajika kujadiliwa katika mkutano huo wa kilele, akiongeza kuwa vikwazo havitatolewa kabla ya wakati huo.Amesema kwa sasa wanaipa nafasi mbinu ya kidiplomasia. Mvutano umezidi kuongezeka kati ya Uturuki na Ugiriki kufuatia jitiahada ya kutafuta mafuta na gesi karibu na eneo la kisiwa cha Cyprus, likionekana kama sehemu ya Ugiriki, ambayo ni taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.,

Umoja wa UIaya unatafakari kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Uturuki kwa sababu ya utafiti wake wa gesi mashariki ya Bahari ya Mediterania, eneo ambalo linagombaniwa na Ugiriki.

Akizungumza baada ya mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya mjini Berlin, Mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borell amesema kutokana na kukosekana kwa maendeleo katika suala hilo, huenda wakatayarisha orodha ya vikwazo zaidi.

Baadae suala hilo litajadiliwa katika mkutano ujao wa kilele Septemba 24. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema kuupanua wigo wa vikwazo dhidi ya Uturuki kutahitajika kujadiliwa katika mkutano huo wa kilele, akiongeza kuwa vikwazo havitatolewa kabla ya wakati huo.

Amesema kwa sasa wanaipa nafasi mbinu ya kidiplomasia. Mvutano umezidi kuongezeka kati ya Uturuki na Ugiriki kufuatia jitiahada ya kutafuta mafuta na gesi karibu na eneo la kisiwa cha Cyprus, likionekana kama sehemu ya Ugiriki, ambayo ni taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *