EU yasema inasimama pamoja na ICC, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 10:00 am

September 4, 2020

Msemaji wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya Peter Stano amesema jumuiya hiyo itaitetea mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kutokana na Marekani kujaribu kuidhoofisha baada ya serikali ya rais Donald Trump kumuwekea vikwazo Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi. Msemaji huyo wa Umoja wa Ulaya, amewaambia waandishi habari mjini Brussels, kwamba jumuiya hiyo haifurahishwi na hatua zinazokwenda kinyume na shughuli za mahakama hiyo. Ufaransa imeitaka Marekani kuondoa vikwazo hivyo dhidi ya Bensouda mara moja.,

Msemaji wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya Peter Stano amesema jumuiya hiyo itaitetea mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kutokana na Marekani kujaribu kuidhoofisha baada ya serikali ya rais Donald Trump kumuwekea vikwazo Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi. 

Msemaji huyo wa Umoja wa Ulaya, amewaambia waandishi habari mjini Brussels, kwamba jumuiya hiyo haifurahishwi na hatua zinazokwenda kinyume na shughuli za mahakama hiyo. Ufaransa imeitaka Marekani kuondoa vikwazo hivyo dhidi ya Bensouda mara moja.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *