EU yafichua mpango wa kupata malighafi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 3, 2020 at 6:00 pm

September 3, 2020

Umoja wa Ulaya umeanzisha leo mkakati mpya wa upatikanaji wa madini muhimu ya kupunguza utegemezi wa nchi zinazotoa madini hayo kama Chile, China na Afrika kusini.Hayo yameelezwa baada ya kuongezeka wasi wasi kuhusiana na utegemezi wa malighafi inayotumika katika kutengeneza simu za mkononi, televisheni na taa zinazotumia nishati ndogo.Umoja wa Ulaya unatarajia kuhitaji kiasi cha mara 60 zaidi ya madini ya lithium na mara 15 zaidi ya cobalti kwa ajili ya magari yanayotumia bateri za umeme na kuhifadhi nishati ifikapo mwaka 2050.Mahitaji yake ya malighafi ya udongo maalum unaotumika katika kutengeneza sumaku kwa ajili ya teknolojia mbali mbali yanaweza kuongezeka mara 10 katika kipindi kama hicho.Janga la virusi vya corona linaonesha ongezeko la utegemezi wa dunia katika vifaa vya elekrotiniki na teknolojia kwa ajili ya kazi kutoka mbali, elimu na mawasiliano, na mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya yanaingia katika mbio zinazozidi kuongezeka katika upatikanaji wa mali hizo kwa ajili ya mawasiliano, afya , ulinzi na sekta za anga pamoja na Marekani, China na Japan.,

Umoja wa Ulaya umeanzisha leo mkakati mpya wa upatikanaji wa madini muhimu ya kupunguza utegemezi wa nchi zinazotoa madini hayo kama Chile, China na Afrika kusini.

Hayo yameelezwa baada ya kuongezeka wasi wasi kuhusiana na utegemezi wa malighafi inayotumika katika kutengeneza simu za mkononi, televisheni na taa zinazotumia nishati ndogo.

Umoja wa Ulaya unatarajia kuhitaji kiasi cha mara 60 zaidi ya madini ya lithium na mara 15 zaidi ya cobalti kwa ajili ya magari yanayotumia bateri za umeme na kuhifadhi nishati ifikapo mwaka 2050.

Mahitaji yake ya malighafi ya udongo maalum unaotumika katika kutengeneza sumaku kwa ajili ya teknolojia mbali mbali yanaweza kuongezeka mara 10 katika kipindi kama hicho.

Janga la virusi vya corona linaonesha ongezeko la utegemezi wa dunia katika vifaa vya elekrotiniki na teknolojia kwa ajili ya kazi kutoka mbali, elimu na mawasiliano, na mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya yanaingia katika mbio zinazozidi kuongezeka katika upatikanaji wa mali hizo kwa ajili ya mawasiliano, afya , ulinzi na sekta za anga pamoja na Marekani, China na Japan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *