EU kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuhusu kupewa sumu Navalny,

October 12, 2020

 

Umoja wa Ulaya umeorodhesha vikwazo dhidi ya maafisa wa Urusi kuhusiana na kupewa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny na dhidi ya kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko kuhusiana na mzozo wa kisiasa nchini mwake. 

Mawaziri wa mambo ya kigeni wanaokutana mjini Luxembourg wamekubaliana kimsingi kuhusu mapendekezo ya vikwazo vilivyotayarishwa na Ufaransa na Ujerumani wiki iliyopita, ambayo yalisema Urusi ilihusika na tukio la Navalny kupewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu aina ya Novichok. 

Kuhusu Belarus, mawaziri hao wamesema wako tayari kumuwekea vikwazo kiongozi wa nchi huyo Lukashenko, wakati umoja huo ukilenga kuongeza mbinyo kwa ukandamizaji unaofanywa na utawala wake dhidi ya waandamanaji. 

Umoja wa Ulaya tayari umeweka vikwazo vya kusafiri na kuzuwia mali za washirika 40 wa Lukashenko kwa wizi wa kura katika uchaguzi wa Agosti ambao ulimrejesha madarakani na kisha akaamuru ukandamizaji dhidi ya maandamano ambayo yameikumba nchi hiyo tangu uchaguzi huo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *