Ethiopia ‘yapiga marufuku safari za anga juu ya bwawa la mto Nile’

October 5, 2020

Ethiopia imepiga marufuku safari za anga katika angala lake juu ya bwana iinalojenga la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) kwasababu za kiusalama, kulingana na tovuti inayomilikiwa na mwanahabari wa kujitegemea.

“Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege la Safari za Anga nchini Ethiopia, Col Wesenyeleh Hunegnaw, amemuambia mwanahabari huyo kwamba kufuatia mashauriano na mashirika husika ya usalama, anga la eneo la jimbo la Benishangul-Gumuz [kaskazini -mashariki mwa Ethiopia] ambapo bwawa hilo linajengwa ni karibu na safari zote za ndege,” ripoti hiyo imesema.

Alisema kwamba hakuna ndege ya abiria au za mizigo zitakazoruhusiwa kusafiri juu ya anga hilo lakini huenda pengine ruhusa ikatolewa kwa atakayewasilisha ombi.

Mkuu wa jeshi la Anga, Meja Jenerali Yilma Merdasa, pia wiki iliyopita alionya kwamba kikosi cha anga kimeboresha ndege zake za kivita na inauwezo wa kulinda bwana hilo kutokana na shambulio lolote la adui.

Bwawa hilo ambalo limezua utata linalotarajiwa kuwa kubwa zaidi Afrika, limeendelea kuzorotesha uhusiano wa Ethiopia na Misri pamoja na Sudan kwa kiasi fulani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *