Ethiopia yamshtaki kongozi wa upinzani kwa makosa ya ugaidi, on September 20, 2020 at 10:00 am

September 20, 2020

 Ethiopia imemfungulia mashitaka kiongozi wake maarufu wa upinzani, Jawar Mohammed, na watu wengine 23 kwa makosa yanayohusiana na ugaidi, ulaghai wa mawasiliano ya simu na uhalifu mwingine. Kama watapatikana na hatia, huenda wakakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imetangaza kuwa washitakiwa watafikishwa mahakamani kesho Jumatatu. Mashitaka hayo yanatokana na machafuko makubwa yaliyozuka Julai katika maeneo ya mji mkuu Addis Ababa, na jimbo la Oromia baada ya kuuawa kwa mwanamuziki Hachalu Hundessa, ambaye alikuwa maarufu katika maandamano ya kuipinga serikali yaliyomuingiza madarakani Waziri Mkuu Abiy Ahmed mwaka wa 2018. Serikali ilisema zaidi ya watu 180 waliuawa katika vurugu hizo za Julai. Jawar, mkosoaji mkubwa wa waziri mkuu, amekuwa kizuizini tangu alipokamatwa wakati wa maandamano ya Julai.,

 

Ethiopia imemfungulia mashitaka kiongozi wake maarufu wa upinzani, Jawar Mohammed, na watu wengine 23 kwa makosa yanayohusiana na ugaidi, ulaghai wa mawasiliano ya simu na uhalifu mwingine. Kama watapatikana na hatia, huenda wakakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani. 

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imetangaza kuwa washitakiwa watafikishwa mahakamani kesho Jumatatu. 

Mashitaka hayo yanatokana na machafuko makubwa yaliyozuka Julai katika maeneo ya mji mkuu Addis Ababa, na jimbo la Oromia baada ya kuuawa kwa mwanamuziki Hachalu Hundessa, ambaye alikuwa maarufu katika maandamano ya kuipinga serikali yaliyomuingiza madarakani Waziri Mkuu Abiy Ahmed mwaka wa 2018. 

Serikali ilisema zaidi ya watu 180 waliuawa katika vurugu hizo za Julai. Jawar, mkosoaji mkubwa wa waziri mkuu, amekuwa kizuizini tangu alipokamatwa wakati wa maandamano ya Julai.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *