Ethiopia yaitaka Marekani kuelezea madai ya kuipunguzia ufadhili, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 3:00 pm

August 31, 2020

Serikali ya Ethiopia inataka ufafanuzi kutoka kwa Marekani kuhusu madai kwamba imepunguza ufadhili wake kwa nchi hiyo mzozo wa ukiendelea kuhusu bwawa kubwa la uzalishaji umeme katika mto Nile.Wiki iliyopita jarida moja linaloangazia sera za kigeni liliripoti kuwa Waziri mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameidhinisha kuzuiliwa kwa msaada wa hadi dola 130 milioni kwa Ethiopia katika juhudi za kuishinikiza ifikie mkataba na Misri kuhusu bwawa hiloKwa karibu muongo mmoja, Ethiopia na Misri zimekuwa zikishauriana kuhusu bwawa hilo.Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.Nchi hizo pamoja na Sudan zinashauriana kuhusu kiwango cha maji kitakachoachiwa kupitia bwawa hiloBalozi wa Ethiopia nchini Marekani, Fitsum Arega, ameandika kati Twitter yake ujumbe uanaosema Marekani imeahidi kutoa maelezo kuhusu suala hilo (18:30 GMT). Lakini hakuna uthibitisho kuwa ufadhili umekatwa.,

Serikali ya Ethiopia inataka ufafanuzi kutoka kwa Marekani kuhusu madai kwamba imepunguza ufadhili wake kwa nchi hiyo mzozo wa ukiendelea kuhusu bwawa kubwa la uzalishaji umeme katika mto Nile.

Wiki iliyopita jarida moja linaloangazia sera za kigeni liliripoti kuwa Waziri mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameidhinisha kuzuiliwa kwa msaada wa hadi dola 130 milioni kwa Ethiopia katika juhudi za kuishinikiza ifikie mkataba na Misri kuhusu bwawa hilo

Kwa karibu muongo mmoja, Ethiopia na Misri zimekuwa zikishauriana kuhusu bwawa hilo.

Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.

Nchi hizo pamoja na Sudan zinashauriana kuhusu kiwango cha maji kitakachoachiwa kupitia bwawa hilo

Balozi wa Ethiopia nchini Marekani, Fitsum Arega, ameandika kati Twitter yake ujumbe uanaosema Marekani imeahidi kutoa maelezo kuhusu suala hilo (18:30 GMT). Lakini hakuna uthibitisho kuwa ufadhili umekatwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *