Erdogan na Merkel wazungumzia mzozo wa mashariki mwa Mediterania, on September 17, 2020 at 8:00 am

September 17, 2020

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake iko tayari kwa mazungumzo ya kuutanzua mzozo baina yake na Ugiriki mashariki mwa bahari ya Mediterania, akisisitiza lakini kuwa nchi yake itaendelea kutetea maslahi yake katika eneo hilo. Hayo ameyaeleza katika mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, yaliyofanyika kwa njia ya video jana jioni. Erdogan amemuambia Merkel kuwa suluhisho linaweza kupatikana kwa njia ya mazungumzo, ili mradi mazungumzo hayo yaendeshwe bila upendeleo. Ujerumani inaongoza katika kuusuluhisha mzozo huo baina ya Ugiriki na Uturuki, nchi mbili wanachama wa umoja wa kujihami wa NATO, ambazo zimetunishiana misuli kwa luteka za kijeshi angani na baharini. Mazungumzo baina ya viongozi hao yamefanyika siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya, ambao utajadili vikwazo dhidi ya Uturuki kama jibu kwa kufanya utafiti katika eneo la bahari linalodaiwa na Ugiriki.,

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake iko tayari kwa mazungumzo ya kuutanzua mzozo baina yake na Ugiriki mashariki mwa bahari ya Mediterania, akisisitiza lakini kuwa nchi yake itaendelea kutetea maslahi yake katika eneo hilo. 

Hayo ameyaeleza katika mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, yaliyofanyika kwa njia ya video jana jioni. 

Erdogan amemuambia Merkel kuwa suluhisho linaweza kupatikana kwa njia ya mazungumzo, ili mradi mazungumzo hayo yaendeshwe bila upendeleo.

 Ujerumani inaongoza katika kuusuluhisha mzozo huo baina ya Ugiriki na Uturuki, nchi mbili wanachama wa umoja wa kujihami wa NATO, ambazo zimetunishiana misuli kwa luteka za kijeshi angani na baharini. 

Mazungumzo baina ya viongozi hao yamefanyika siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya, ambao utajadili vikwazo dhidi ya Uturuki kama jibu kwa kufanya utafiti katika eneo la bahari linalodaiwa na Ugiriki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *