Elsa Majimbo: Mchekeshaji wa Kenya apewa mkataba kukuza nembo ya fesheni ya Rihanna Fenty

September 14, 2020

Dakika 4 zilizopita

Elisha majimbo

Mchekeshaji wa kula viazi Elsa majimbo ambaye alijipatia umaarufu kwa hotuba zake katika mtandao wa twitter na Instagram tangu kuanza kwa mlipuko wa corona amefanikiwa kuingia mkataba na nembo ya fesheni ya Rihanna kwa jina Fenty.

Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alisema kwamba anajivunia mkataba wake wa kukuza nembo hiyo ya Rihanna.

Nembo hiyo ya Rihanna ilituma ujumbe wa ukanda wa video katika mtandao wa twitter ambapo ilitangaza mpango huo.

”Naishukuru familia ya fenty wamekuwa watu wazuri pamoja na Rihanna katika nembo hii”, Elsa alituma ujumbe wa twitter.

Kanda zake za video alizopiga chumbani mwake mjini Nairobi zimewavutia watazamaji wengi barani Afrika .

Anakula viazi huku akiwa ametegemea mto wake wakati akizungumza, kabla ya kuficha uso kwa kuvalia miwani meusi.

Kanda zake za video zimevutia makumi ya maelfu ya watazamaji katika mitandao ya kijamii.

Katika maelezo yake mafupa alioandika katika mtandao wake wa YouTube anasema kwamba anatumia simu aina ya iphone 6 kupiga video hizo.

Mwezi Julai , aliambia gazeti la Uingereza The Guradian kwamba familia yake haipendi video zake lakini sasa wameanza kuzipenda polepole.

Alisema kwamba katika siku za baadaye atafanya uigizaji na kusoma kidogo – ni mwandishi katika chuo kikuu cha Strathmore jijini Nairobi.

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, Elisha/ Twitter Mchekeshaji wa kula viazi Elsa majimbo ambaye alijipatia umaarufu kwa hotuba zake…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *