Ecowas inatumai utawala wa kiraia utarejea Mali ‘ ndani ya siku kadhaa’, on September 16, 2020 at 1:00 pm

September 16, 2020

Rais wa Ghana, Nana Akufo- Addo, amesema viongozi wa magharibi mwa Afrika wanamatumaini ya kuiona serikali inayoongozwa na raia ikiwekwa nchini Mali katika kipindi cha siku kadhaa.Alizungumza baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa kikanda na na wanamgambo wa Junta ambao walichukua mamlaka nchini mali mwezi uliopita.Bwana Akufo- Addo alisema kuwa jumuiya ya kiuchumi ya nchi zilizoko magharibi mwa Afrika Ecowas, wataondoa vikwazo ” mara moja ” pale raia watakapochukua mamlaka nchini Mali.Viongozi wa Ecowas walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mazungumzo juu ya mzozo wa kisasa wa Mali.Viongozi wa jeshi la Mali junta, Kanali Assimi Goita, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pia walihudhuria.Viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanahofia kwamba hali ya usalama nchini Mali inaweza kuhaibiwa zaidi na kudhoofishwa kwa juhudi zilizofanyika kuyashinda makundi ya wapiganaji wa kiislamu.Jumamosi, upinzani unaofahamika kama M5-RFP ulipinga pendekezo la jeshi la mchakato wa kipindi cha mpito cha miezi 18.,

Rais wa Ghana, Nana Akufo- Addo, amesema viongozi wa magharibi mwa Afrika wanamatumaini ya kuiona serikali inayoongozwa na raia ikiwekwa nchini Mali katika kipindi cha siku kadhaa.

Alizungumza baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa kikanda na na wanamgambo wa Junta ambao walichukua mamlaka nchini mali mwezi uliopita.

Bwana Akufo- Addo alisema kuwa jumuiya ya kiuchumi ya nchi zilizoko magharibi mwa Afrika Ecowas, wataondoa vikwazo ” mara moja ” pale raia watakapochukua mamlaka nchini Mali.

Viongozi wa Ecowas walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mazungumzo juu ya mzozo wa kisasa wa Mali.

Viongozi wa jeshi la Mali junta, Kanali Assimi Goita, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pia walihudhuria.

Viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanahofia kwamba hali ya usalama nchini Mali inaweza kuhaibiwa zaidi na kudhoofishwa kwa juhudi zilizofanyika kuyashinda makundi ya wapiganaji wa kiislamu.

Jumamosi, upinzani unaofahamika kama M5-RFP ulipinga pendekezo la jeshi la mchakato wa kipindi cha mpito cha miezi 18.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *