e Katibu Mkuu Wa Mambo Ya Nje Afanya Mazungumzo Na Mratibu Mkazi Wa Umoja Wa Mataifa Nchini, noreply@blogger.com (Unknown), on September 3, 2020 at 10:05 am

September 3, 2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Bw. Zlatan Milišić alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa upande wake, Bw. Milišić aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa nchi kustawi. Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye mataifa mbalimbali  yenye  migogoro duniani na kuitakia Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020.,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,

Bw. Zlatan Milišić alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.

Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Kwa upande wake, Bw. Milišić aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa nchi kustawi.

 Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye mataifa mbalimbali  yenye  migogoro duniani na kuitakia Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *