Dude apata ajali, akimbizwa Hospitalini, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 28, 2020

Msanii wa filamu Bongo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amekimbizwa Hospitali ya Magomeni Jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya bodaboda kwa kugongwa na gari la kubebea wagonjwa Ambulance.Katibu wa wasanii wa filamu Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha kichwani.”Kwa sasa tupo Hospitali Magomeni, alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na Ambulance yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali, mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo” ameeleza Katibu wa wasanii Jafari Makatu ,

Msanii wa filamu Bongo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amekimbizwa Hospitali ya Magomeni Jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya bodaboda kwa kugongwa na gari la kubebea wagonjwa Ambulance.

Katibu wa wasanii wa filamu Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha kichwani.

“Kwa sasa tupo Hospitali Magomeni, alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na Ambulance yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali, mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo” ameeleza Katibu wa wasanii Jafari Makatu 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *