DK Shein anena haya kwenye ufunguzi wa Kampeni, on September 12, 2020 at 5:00 pm

September 12, 2020

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein alisema kwamba mgombea urasi wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mgombea urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  wote kwa ujumla  wanakila sababu ya kuongoza Zanzibar na Tanzania kutokana kuwa na sifa zilizotukuka katika utendaji wao wa kazi.Hayo ameyasema leo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM ambazo zimefanyika katika viwanja vya Demokrasia kibanda maiti Mkoa wa Mjini Unguja, Uzinduzi huo umehudhuriwa na maelfu ya wapenzi na wanachama wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali ya visiwa vya Zanzibar.Alisema, Dk Hussein Ali Mwinyi ana kila sifa za kuiongoza Zanzibar kwa kuwa Rais wa Zanzibar kwani ana uwezo mkubwa sana na sio mwanagenzi katika siasa kwani ameshawahi kuongoza katika majimbo mawili akiwa mbunge likiwemo Jimbo la Mkuranga na la kwa hani.Alisema, alisema anamfahamu vizuri Dk Mwinyi na ana uwezo mkubwa wa kuiongoza Zanzibar na ndio maana chama kimemteua kuweza kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia chhama hicho.Alifahamisha kuwa, Dk Mwinyi ana uwezo mkubwa sana kwani taaluma yake ni Daktari bingwa wa binaadamu na ni mtu aliyesoma akabobea na ni muhadhiri wa chuo kikuu.”Dk Mwinyi ana uwezo mkuwa sana, ana upeo na ndio maana CCM ikamchagua aiongoze Zanzibar, lakini ana heshia kubwa  kwa wkubwa zake na wadogo zake, na anajiheshimu mwenyewe sijawahi kusikia wala kuhadisiwa kumvunjia mtu heshima yake,” alisemaKatika Ufunguzi huo wa kampeni wasanii mbali mbali wa filamu, Bongo fleva pamoja na vikundi mbalimbali vyataarabu kutoka Zanzibar na Bara vimewaburudisha wanachama wa chama hicho.,

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein alisema kwamba mgombea urasi wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mgombea urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  wote kwa ujumla  wanakila sababu ya kuongoza Zanzibar na Tanzania kutokana kuwa na sifa zilizotukuka katika utendaji wao wa kazi.

Hayo ameyasema leo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM ambazo zimefanyika katika viwanja vya Demokrasia kibanda maiti Mkoa wa Mjini Unguja, Uzinduzi huo umehudhuriwa na maelfu ya wapenzi na wanachama wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali ya visiwa vya Zanzibar.

Alisema, Dk Hussein Ali Mwinyi ana kila sifa za kuiongoza Zanzibar kwa kuwa Rais wa Zanzibar kwani ana uwezo mkubwa sana na sio mwanagenzi katika siasa kwani ameshawahi kuongoza katika majimbo mawili akiwa mbunge likiwemo Jimbo la Mkuranga na la kwa hani.

Alisema, alisema anamfahamu vizuri Dk Mwinyi na ana uwezo mkubwa wa kuiongoza Zanzibar na ndio maana chama kimemteua kuweza kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia chhama hicho.

Alifahamisha kuwa, Dk Mwinyi ana uwezo mkubwa sana kwani taaluma yake ni Daktari bingwa wa binaadamu na ni mtu aliyesoma akabobea na ni muhadhiri wa chuo kikuu.

“Dk Mwinyi ana uwezo mkuwa sana, ana upeo na ndio maana CCM ikamchagua aiongoze Zanzibar, lakini ana heshia kubwa  kwa wkubwa zake na wadogo zake, na anajiheshimu mwenyewe sijawahi kusikia wala kuhadisiwa kumvunjia mtu heshima yake,” alisema

Katika Ufunguzi huo wa kampeni wasanii mbali mbali wa filamu, Bongo fleva pamoja na vikundi mbalimbali vyataarabu kutoka Zanzibar na Bara vimewaburudisha wanachama wa chama hicho.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *