DK Msuya atinga Mwanga kumuombea kura Dk Magufuli na Thadayo “CCM Baba lao”, on September 7, 2020 at 6:48 am

September 7, 2020

ALIYEKUA mtia nia kupitia wa Ubunge Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk Ombeni Msuya amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli na mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Joseph Thadayo.Dk Msuya ametoa kauli hiyo alipofika kumnadi Thadayo katika kampeni za ubunge jimbo la Mwanga ambapo amesema yeye na wenzake 53 ambao waligombea pamoja na Thadayo wataendelea kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na chama.Amesema yeye ni kijana aliyelelewa ndani ya CCM hivyo maamuzi yaliyotolewa na chama kumpitisha Thadayo anayaheshimu kwa sababu ni ya kidemokrasia na atatumia nguvu na akili zake kuhakikisha Jimbo la Mwanga linabaki CCM na wanaibuka na ushindi wa kura nyingi.” Sisi bado ni vijana hivyo ni jukumu letu kuunganisha nguvu zetu wote ili tuweze kupata kura nyingi za mgombea wetu wa Urais, Dk John Magufuli, mgombea wetu wa Ubunge na Madiwani wote wa kata 20.Rais wetu amefanya mambo makubwa sana, miradi aliyoianzisha ndani ya Nchi yetu imekua ajira kwa maelfu ya watanzania wenzetu, usafiri wa Treni huku Kaskazini tulishausahau lakini Dk Magufuli ameurudisha, hakika anastahili mitano tena,” Amesema Dk Msuya.Dk Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema CCM Wilaya ya Mwanga haina makundi na sasa akili yao ni kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.” Hakuna makundi Mwanga, lengo letu ni moja tu kuhakikisha Dk Magufuli anapata kura za kishindo, mgombea wetu wa Ubunge anaibuka mshindi na Halmashauri yetu inaundwa na madiwani wa CCM, hivyo niwaombe wananchi wote Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi tukawaoneshe wapinzani kwamba Nchi hii CCM ndo Baba lao,” Amesema Dk Msuya.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge mstaafu wa Mwanga, Cleopa Msuya ambaye aliwasihi wana CCM wote kuungana na kushirikiana katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na kueleza mafanikio yote yaliyofanywa na Rais Magufuli ndani ya kipindi chake cha miaka mitano.,

ALIYEKUA mtia nia kupitia wa Ubunge Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk Ombeni Msuya amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli na mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Joseph Thadayo.

Dk Msuya ametoa kauli hiyo alipofika kumnadi Thadayo katika kampeni za ubunge jimbo la Mwanga ambapo amesema yeye na wenzake 53 ambao waligombea pamoja na Thadayo wataendelea kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na chama.

Amesema yeye ni kijana aliyelelewa ndani ya CCM hivyo maamuzi yaliyotolewa na chama kumpitisha Thadayo anayaheshimu kwa sababu ni ya kidemokrasia na atatumia nguvu na akili zake kuhakikisha Jimbo la Mwanga linabaki CCM na wanaibuka na ushindi wa kura nyingi.

” Sisi bado ni vijana hivyo ni jukumu letu kuunganisha nguvu zetu wote ili tuweze kupata kura nyingi za mgombea wetu wa Urais, Dk John Magufuli, mgombea wetu wa Ubunge na Madiwani wote wa kata 20.

Rais wetu amefanya mambo makubwa sana, miradi aliyoianzisha ndani ya Nchi yetu imekua ajira kwa maelfu ya watanzania wenzetu, usafiri wa Treni huku Kaskazini tulishausahau lakini Dk Magufuli ameurudisha, hakika anastahili mitano tena,” Amesema Dk Msuya.

Dk Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema CCM Wilaya ya Mwanga haina makundi na sasa akili yao ni kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

” Hakuna makundi Mwanga, lengo letu ni moja tu kuhakikisha Dk Magufuli anapata kura za kishindo, mgombea wetu wa Ubunge anaibuka mshindi na Halmashauri yetu inaundwa na madiwani wa CCM, hivyo niwaombe wananchi wote Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi tukawaoneshe wapinzani kwamba Nchi hii CCM ndo Baba lao,” Amesema Dk Msuya.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge mstaafu wa Mwanga, Cleopa Msuya ambaye aliwasihi wana CCM wote kuungana na kushirikiana katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na kueleza mafanikio yote yaliyofanywa na Rais Magufuli ndani ya kipindi chake cha miaka mitano.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *