Dk Ali Mohammed Shein aagwa baada ya miaka 10 uongozini

October 19, 2020

Akizungumza katika hafla hiyo Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amesema mipango ya nchi haiwezi kufikiwa kama hakuna dira ya maendeleo na amewataka wataalamu kufanya tathmini ili kubaini kasoro zilizopo na kuzifanyia kazi ili dira hiyo iwe na mafanikio, na kuisifu Zanzibar kuwa ina uwezo mkubwa.

Akizungumzia lengo la Dira hiyo Kamishna wa bajeti Zanzibar Bwana Mwita Mgeni Mwita alisema Dira ya maendeleo ya 2050 imejikita katika kuwawezesha watu katika nyanja zote pamoja na maendeleo yao.

Lengo ni kuifikisha Zanzibar katika uchumi wa kati wa kiwango cha juu sawa na kipato cha mwananchi 4,400.

Dira imefanywa kwa ushirikiano wa wataalamu mbalimbali wa ndani na wenyewe wazanzibari kuanza mwanzo hadi mwisho ambayo lengo lake ni kufikisha kiwango cha kati cha uchumi.

Pendekezo la kuandaliwa Dira ya maendeleo liliasisiwa mwishoni mwa mwaka ya 1990 ambapo Jumuiya za Kimataifa zilikubaliana na nchi kadhaa kuandaa mipango ya muda mrefu ili isaidie kwa kupunguza viwango vya umasikini duniani.

Baadhi ya nchi zilifuata utaratibu huo ikiwemo Zanzibar ambayo Dira ya Maendeleo ya 2025 na sasa 2050, Tanzania bara iliandaa ya miaka mitano 2025 na Kenya Dira ya 2030.

Mwandishi: Salma Said DW Zanzibar

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *