Ditopile awashukia wanaofanya mauaji kwa wana CCM, Awaomba viongozi wa Dini kukemea,

October 6, 2020

Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amefanya mkutano wa kuomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli katika Kata ya Hogoro wilayani Kongwa ambapo amelaani vitendo vya kujeruhiwa na kuuawa kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kinachofanywa na vyama pinzani.

” Hadi sasa vijana wetu wa nne wameshauawa na vyama vya upinzani, tumeshuhudia Iringa, Tunduma na hapa Chemba Dodoma. Tuwapongeze Jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua lakini tunaungana na Katibu Mkuu wetu, Dk Bashiru Ally kukemea vitendo hivi na kuwasihi watanzania kuwaepuka watu wenye lengo la kutugawa na kuumiza maisha ya watanzania wenzetu,

Watu hawa ni wa hovyo, wanaomba kuongoza Nchi lakini wametawaliwa na chuki, Mgombea wao wa Urais kule Zanzibar anahubiri Udini na kuhamasisha vitendi vya kuumiza watu, ivi karibuni wamevamia watu wetu Msikitini na kuwaumiza,  tusiwachague watu wa namna hii watatugawa.

Tuwapongeze Jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua lakini tunaungana na Katibu Mkuu wetu, Dk Bashiru Ally kukemea vitendo hivi na kuwasihi watanzania kuwaepuka watu wenye lengo la kutugawa na kuumiza maisha ya watanzania wenzetu,” Amesema Ditopile.

Amewaomba watanzania na hasa viongozi wa Dini kukemeea mauaji hayo na vitendo hivyo na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kumpigia kura Dk Magufuli ili aweze kuibuka na ushindi wa kishindo na kuwatumikia watanzania kwa miaka mingine mitano.

” Wote mmeshuhudiwa kule Iringa viongozi wa Chadema wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya wana CCM wenzetu, kwa vitendo wanavyovifanya wanaonesha jinsi gani hawafai kupewa madaraka kwani watavunja amani ya Nchi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *