Ditopile amvaa Sheikh Ponda “Amenajisi cheo cha Sheikh, anatumika kuvuruga amani”,

October 19, 2020

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amemshukia Sheikh Issa Ponda kuwa anatumika na vikundi vya kigaidi na msimamo alioutoa juu ya Waislamu kumuunga mkono Lissu ni batili na umelenga kuchochea machafuko jambo ambalo halikubaliki. Ditopile ameyasema hayo kwenye kampeni za CCM kata ya Makole, Dodoma Mjini.

” Sheikh Ponda anatia najisi cheo cha Sheikh, anasema Waislamu wote wanaiunga mkono Chadema mbona mimi sitoipigia kura Chadema, tunapaswa kuwaepuka wapinzani hapa hawajachukua Nchi wameshaanza kutugawa kwa Imani za Dini tukiwapa Nchi si watatutawala kidini? CCM pekee ndio chama kinachoongoza kwa misingi ya haki na Uhuru wa kuabudu bila kutugawa kidini na kikabila.

Dk Magufuli licha ya kuwa Mkristo lakini amesaidia kutujengea Waislamu Msikiti mkubwa Afrika Mashariki, huyu ndio Rais asiye na ubaguzi. Ponda vikundi vya kigaidi vinavyomtumia tunavijua, Serikali ya CCM chini ya Jemedari Dk Magufuli haipp tayari kuruhusu wananchi wake wapate shida, Waislamu hatulitambua tamko la Ponda kwa sababu yeye siyo msemaji wetu bali mtu mwenye kuchochea ubaguzi na hafai kwenye jamii yetu,” Amesema Ditopile.

Katika mkutano huo Ditopile amewataka watanzania kuwaepuka viongozi wachonganishi waliotawaliwa na tamaa za madaraka kiasi cha kutaka hata kuwagawa watanzania kwa kutumia Dini.

Ditopile amewaomba wananchi wa kata ya Makole kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kumpigia kura za ushindi mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na mgombea udiwani wa kata hiyo,

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *