Ditopile ampa makavu mgombea Ubunge wa Chemba kupitia Chadema, on September 13, 2020 at 5:00 pm

September 13, 2020

MBUNGE mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ditopile ameshiriki kampeni mbili tofauti leo ikiwa ni muendelezo wa kutafuta kura za wagombea wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.Ditopile ameshiriki kampeni za Ubunge Jimbo la Chemba, Dodoma ambazo zimezinduliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kisha baadae kuzindua kampeni za udiwani Kata ya Mihuji na kumnadi mgombea wake, Beatrice Ngerangera.Akizungumza katika mkutano wa kampeni Chemba mbele ya Waziri Mkuu, Ditopile amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea Ubunge, Mohammed Monni na madiwani wote wa chama hicho ili waweze kushirikiana kuweza kuwaletea maendeleo.Ditopile amesema mgombea wa upinzani kupitia Chadema, katika mkutano wake alitoa lugha chafu za kuwakejeli wananchi wa Chemba haswa wanaume na kuwaomba kumjibu kwa kutompigia kura yeye na Chama chake na kuwapigia kura nyingi za kishindo wagombea wa CCM wakiongozwa na Dk Magufuli.” Huyu mgombea wa upinzani namfahamu vizuri sana, ni mtu ambaye hawezi kuleta maendeleo hapa Chemba, amefanya uwekezaji wake binafsi katika majimbo mengine kama angekua anawapenda si angeleta biashara zake hapa ili ziwe msaada kwa vijana wa Chemba na kukuza uchumi wenu?Amewatukana na kuwakejeli wanaume wa Chemba kwa kuwaambia hawana kitu, twendeni Oktoba 28 kwa wingi tukamjibu kwenye boksi la kura,” Amesema Ditopile.Amesema Chemba imenufaika na serikali ya Dk Magufuli kwa kujengewa vituo vitatu vya afya ambavyo vitaondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu huku akimshukuru pia Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa ambaye aliahidi kuwa Chemba itajengewa Hospitali ya Wilaya ambayo itagharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.8.Ditopile pia amezindua kampeni za Udiwani Kata ya Mihuji iliyopo Jimbo la Dodoma Mjini ambapo amemnadi mgombea Udiwani, Beatrice Ngerangera huku akiwaomba wananchi wa kata hiyo kuwapigia kura mafiga matatu ya CCM ambayo ni Mgombea Urais, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge, Anthony Mavunde na Diwani.” ” Kata ya Mihuji ina changamoto zake na mtu pekee anaezijua changamoto za hapa ni Beatrice Ngerangera, niwaombe ndugu zangu wa hapa mchagueni Rais Magufuli, Mbunge Mavunde na Diwani Beatrice ili waweze kushirikiana kuweza kuwaletea maendeleo kwa haraka,” Amesema Ditopile.,

MBUNGE mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ditopile ameshiriki kampeni mbili tofauti leo ikiwa ni muendelezo wa kutafuta kura za wagombea wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Ditopile ameshiriki kampeni za Ubunge Jimbo la Chemba, Dodoma ambazo zimezinduliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kisha baadae kuzindua kampeni za udiwani Kata ya Mihuji na kumnadi mgombea wake, Beatrice Ngerangera.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni Chemba mbele ya Waziri Mkuu, Ditopile amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea Ubunge, Mohammed Monni na madiwani wote wa chama hicho ili waweze kushirikiana kuweza kuwaletea maendeleo.

Ditopile amesema mgombea wa upinzani kupitia Chadema, katika mkutano wake alitoa lugha chafu za kuwakejeli wananchi wa Chemba haswa wanaume na kuwaomba kumjibu kwa kutompigia kura yeye na Chama chake na kuwapigia kura nyingi za kishindo wagombea wa CCM wakiongozwa na Dk Magufuli.

” Huyu mgombea wa upinzani namfahamu vizuri sana, ni mtu ambaye hawezi kuleta maendeleo hapa Chemba, amefanya uwekezaji wake binafsi katika majimbo mengine kama angekua anawapenda si angeleta biashara zake hapa ili ziwe msaada kwa vijana wa Chemba na kukuza uchumi wenu?

Amewatukana na kuwakejeli wanaume wa Chemba kwa kuwaambia hawana kitu, twendeni Oktoba 28 kwa wingi tukamjibu kwenye boksi la kura,” Amesema Ditopile.

Amesema Chemba imenufaika na serikali ya Dk Magufuli kwa kujengewa vituo vitatu vya afya ambavyo vitaondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu huku akimshukuru pia Mjumbe wa Kamati Kuu, Kassim Majaliwa ambaye aliahidi kuwa Chemba itajengewa Hospitali ya Wilaya ambayo itagharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.8.

Ditopile pia amezindua kampeni za Udiwani Kata ya Mihuji iliyopo Jimbo la Dodoma Mjini ambapo amemnadi mgombea Udiwani, Beatrice Ngerangera huku akiwaomba wananchi wa kata hiyo kuwapigia kura mafiga matatu ya CCM ambayo ni Mgombea Urais, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge, Anthony Mavunde na Diwani.

” ” Kata ya Mihuji ina changamoto zake na mtu pekee anaezijua changamoto za hapa ni Beatrice Ngerangera, niwaombe ndugu zangu wa hapa mchagueni Rais Magufuli, Mbunge Mavunde na Diwani Beatrice ili waweze kushirikiana kuweza kuwaletea maendeleo kwa haraka,” Amesema Ditopile.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *