Ditopile aeleza mafanikio ya Magufuli kwenye sekta ya Afya Kondoa, on September 9, 2020 at 10:00 am

September 9, 2020

 KATIKA kuendelea kutafuta kura za mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wabunge na Madiwani, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameshiriki uzinduzi wa kampeni Jimbo la Kondoa Mji na kuiombea kura CCM.Ditopile amewaomba wananchi wa Kondoa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Makoa Ally pamoja na madiwani wote ili waweze kushughulika na shida ya maji inayowakabili wananchi wa Kondoa.Amesema ndani ya miaka mitano ya Dk Magufuli Wilaya ya Kondoa imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo ikiwemo kujengewa miundombinu ya barabara, maboresho katika sekta ya Afya.” Wote ni mashahidi hii barabara ya kutoka Kondoa kwenda Dodoma ilikua haipitiki, tungeweza kusafiri masaa hadi nane kutoka Kondoa hadi Dodoma mjini tena kwa gari, lakini leo ni masaa mawili tu umefika, yote haya ni kwa sababu ya Dk Magufuli.Wilaya hiyo ilikua na shida kwenye eneo la afya, lakini Rais wetu alivyoingia miaka mitano tu tumejengewa vituo sita vya afya tena vya kisasa na vyenye ubora wa Hospitali za Wilaya, kwenye elimu nyinyi wote ni mashahidi sasa watoto wetu wanasoma bure kuanzia elimu ya Msingi hadi kidato cha nne,” Amesema Ditopile.Amewaomba wananchi wote kujitokeza Oktoba 28 kwenda kupiga kura za Ndio kwa CCM ili kumpa ushindi mkubwa Dk Magufuli aweze kumalizia kazi aliyokwisha kuianza ya kuwaletea maendeleo watanzania ikiwemo Kondoa.,

 

KATIKA kuendelea kutafuta kura za mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wabunge na Madiwani, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameshiriki uzinduzi wa kampeni Jimbo la Kondoa Mji na kuiombea kura CCM.

Ditopile amewaomba wananchi wa Kondoa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Makoa Ally pamoja na madiwani wote ili waweze kushughulika na shida ya maji inayowakabili wananchi wa Kondoa.

Amesema ndani ya miaka mitano ya Dk Magufuli Wilaya ya Kondoa imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo ikiwemo kujengewa miundombinu ya barabara, maboresho katika sekta ya Afya.

” Wote ni mashahidi hii barabara ya kutoka Kondoa kwenda Dodoma ilikua haipitiki, tungeweza kusafiri masaa hadi nane kutoka Kondoa hadi Dodoma mjini tena kwa gari, lakini leo ni masaa mawili tu umefika, yote haya ni kwa sababu ya Dk Magufuli.

Wilaya hiyo ilikua na shida kwenye eneo la afya, lakini Rais wetu alivyoingia miaka mitano tu tumejengewa vituo sita vya afya tena vya kisasa na vyenye ubora wa Hospitali za Wilaya, kwenye elimu nyinyi wote ni mashahidi sasa watoto wetu wanasoma bure kuanzia elimu ya Msingi hadi kidato cha nne,” Amesema Ditopile.

Amewaomba wananchi wote kujitokeza Oktoba 28 kwenda kupiga kura za Ndio kwa CCM ili kumpa ushindi mkubwa Dk Magufuli aweze kumalizia kazi aliyokwisha kuianza ya kuwaletea maendeleo watanzania ikiwemo Kondoa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *