Director Ivan kulipwa mkwanja mrefu na Navy Kenzo

October 2, 2020

 

 Director Ivan amewasifu wasanii wa kundi la Navy Kenzo ambo ni Aika na Nahreel, kwa kusema ni watu ambao wapo makini na kazi yao pia hawana ubabaishaji katika suala zima la ulipaji wa pesa kama walivyo wasanii wengine.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Director Ivan amesema kuwa Navy Kenzo waliweza kumlipa vizuri kuanzia pesa ya kazi hadi gharama za eneo la kufanyia video.

“NavyKenzo hawana mambo mengi wanataka kila mlichopanga ndiyo kifanyike kwa wakati, pia wapo makini na kazi yao kwenye upande wa location pekee wamelipa dola 2000 sawa na milioni 4 na Laki 6, wasanii wengi wanaishia Dola 500 au 800″ amesema Director Ivan

“Ilifika muda nikahisi kila mtu ananiamini na natarajia kufanya kazi na Director wengine wa Marekani, hapa Bongo ukiniuliza msanii anayeniamini lazima nitamtaja Lady Jay Dee kwa sababu ndiye msanii ambaye alijitokeza kuniamini” ameongeza

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *