Dinosaria mwenye vidole viwili tu asiye na meno apatikana

October 18, 2020

Dakika 8 zilizopita

Oksoko avarsan

Maelezo ya picha,

Kiumbe hicho chenye manyoya kilikuwa na mdomo mkubwa, asiye na meno na mwenye vidole viwili tu

Spishi mpya ya dinosaria asiye na meno na mwenye vidole viwili pekee katika kila mkono amebainika kwenye jangwa la Gobi nchini Mongolia.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Edinburgh kilibaini mifupa kadhaa ya spishi hiyo waliopewa jina la Oksoko avarsan.

Kiumbe hicho chenye manyoya ambacho kinasemekana kiliishi miaka milioni 100 iliyopita, pia kilikuwa na mdomo mrefu, mkubwa.

Timu husika ilisema ufumbuzi huo unaweza kusaidia kuelezea vile wanyama wanavyopoteza vidole vya mikononi na miguuni kupitia mabadiliko ya spishi.

Walisema kwamba spishi hiyo ilipungua kidole kimoja mkononi ikilinganishwa na wanyama wa karibu nae.

Bucket of bones

Maelezo ya picha,

Watafiti wa Chuo kikuu cha Edinburgh walipata mifupa kadhaa ya shpihi hii mpya iliyopewa jina la Oksoko avarsan

Wanyama hao ambao walikua hadi urefu wa mita mbili, midomo yao ilifanana na ya kasuku.

Timu hiyo ilisema kwamba uvumbuzi wa kuwa dinosaria hao walibadilika miguu yao ya mbele kunaashiria waliweza kubadilisha lishe na maisha yao na wakaruhusu utofauti na hata kuzaliana.

Mabaki ya dinosaria hao wanne wadogo yalihifadhiwa pamoja.

Scale of dinosaur

Maelezo ya picha,

Ukubwa wa dinosaria ulikuwa nusu ya mwanadamu

Dr Gregory Funston, of the University of Edinburgh’s school of geosciences, said the discovery shed light on how a group of parrot-like animals thrived more than 68 million years a

“Oksoko avarsan – spishi hii inafurahisha kwasababu mifupa yao iko kamili na vile walivyohifadhiwa pamoja kunaonesha namna viumbe hao walivyokuwa wakitembea kwa makundi.

“Lakini cha muhimu zaidi, mkono wenye vidole viwili kulitufanya tuangalie mkono na miguu ya mbele ilivyobadilika katika kipindi chote cha mabadiliko ya maumbile ambako kulikuwa hakujawahi kufanyika hapo kabla”.

Uchunguzi wa dinosaria hao ulijumuisha watafiti kutoka chuo cha Alberta na makumbusho ya dinosaria ya Philip J Currie nchini Canada, chuo kikuu cha Hokkaido nchini Japan na chuo cha sayansi cha Mongoli.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *