Diddy azindua chama kipya cha siasa cha watu weusi,

October 19, 2020

 

Rapper mkongwe kutoka Marekani, Sean John Combs maarufu kama Diddy mishoni mwa wikiendi amezindua chama kipya cha siasa cha watu weusi alichokipa jina la ‘Our Black Party’ ambacho kitakuwa kwa ajili ya kuendeleza ajenda inayozingatia mahitaji ya jamii ya watu weusi.

Diddy ambaye ni mmiliki wa lebo ya Bad Boys Entertainment, lakini pia ni mmoja kati ya wasanii matajiri duniani akiwa mpaka sasa anautajiri wa zaidi ya dola milioni 885, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika..

“Kwa hivyo, nazindua moja ya mambo ya ujasiri zaidi ambayo nimewahi kuzindua. Ninazindua chama cha siasa cha Weusi na vijana wengine waliochaguliwa kuwa viongozi weusi na wanaharakati. Kinaitwa Ourblackparty, haijalishi kama wewe ni Republican au Democrat” – Diddy.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *