Denson azindua kampeni ya kishindo Sirari,

October 3, 2020

Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea udiwani kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Denson John Makanya jana amezindua kampeni za uchaguzi kwa kishindo.

Mgombea udiwani huyo anagombea ndani ya  kata ya Sirari ambapo alisema kuwa wapiga kura wamwamini na kumpa kura zote za ndio ili kuwaletea maendeleo.

Makanya alitaja vipaumbele atakavyoanza navyo kuwa ni pamoja na huduma za jamii ikiwemo miundombinu ya barabara ambapo atahakikisha kuwa zinapitika na wananchi wanasafiri kwa urahisi.

Makanya aliongeza kuwa kipaumbele chake kingine atahakikisha kuwa Sirari inakuwa na amani na wakazi wa maeneo hayo ya ujirani mwema Tanzania na Kenya  wanatemeleana  kwa kufuata taratibi za kisheria.

“Niwahakikishie ndugu zangu mkinipa ridhaa ya kuwa diwani nitaenda kusimamia Amani,kusimamia shuguli za kijamii wagomjwa mpate madwa,na pia nitaenda kutenda haki kwa kila moja simnajua”alisema Makanya.

Makanya alitumia nafasi hiyo kupongeza Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC kwa kurudisha jina lake ambapo hapo awali lilikuwa limewekewa pingamizi kuwa yeye ni Mkenya.

Kwa upande wake Chacha Heche alisema kuwa Chama cha Chadema kitaenda kufanya kampeni za kistaarabu kwa mjibu wa sheria za nchi na maelekezo ya Tume ya uchaguzi ili kujiletea sifa ya kujizolea kura kwa wagombea wakengazi ya Urais,Ubunge na madiwani.

Heche alitumia nafasi hiyo kumnadi Denson mgombea udiwani kata ya sirari ili wapiga kura wampatie kura nyingi za kutosha na kuwa mwakilishi wao pia aliomba wapiga kura kumchagua John Heche kuwa Mbunge wa Tarime vijijini pamoja na kumpa mgombe urais Tundu Lissu kura za kutosha na kuwa Rais ili  kuunda baraza la mawaziri. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *