DC Njombe ashauri halmashauri kujenga kituo cha kulea wazee wa kiume,

October 3, 2020

Na Amri KilagalilaNjombe

Wazee 1051 wa halmashauri ya mji wa Njombe kati 7583, wanawake wakiwa 4092 na wanaume 3491 wamepata vitambulisho vya huduma ya afya kama sera ya afya inavyoagiza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya na kuwawezesha kupata matibabu mahali popote.

Ni katika kutekeleza sera ya wizara ya afya ili kuwasaidia wazee kupata huduma za afya bure ambapo mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameongoza zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wazee 80 na kufikia idadi ya 1051 ambapo kutokana na changamoto wanazo pitia ameshauri halmashauri ya mji wa Njombe  kwa kushirikiana na wadau kujenga kituo cha kutunza wazee wa kiume kwa kuwa upande wa akna mama tayari wameweza kuwa na kituo.

“Niombe mkurugenzi ashirikiane na taasisi zingine akae nazo na mimi niweze kushirikiana naye ili tuone uwezekano wa kutafuta kiwanja tufanye harambee ili tuhakikishe na wazee nao wanapata sehemu ya kuishi”

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Njombe Iluminatha Mwenda amesema kuwa halmashauri hiyo licha ya kutoa huduma za afya bure kwa wazee pia halmashauri imekuwa ikitoa mikopo kwa wazee kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Kwa upande wao wazee waliopatiwa vitambulisho hivyo bure wameishukuru serikali kwa madai kuwa uwepo wa bima unaweza kusaidia kurefusha maisha yao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *