DC Ngubiagai atilia shaka korosho chafu kurejeshwa sokoni, ucheleweshaji vifungashio na ahadi za taasisi za fedha kwa wakulima, on September 18, 2020 at 1:00 pm

September 18, 2020

Na Ahmad Mmow, Lindi.Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai ameonesha mashaka kuhusu hatima ya korosho daraja la tatu( Gredi kutupa) kurejea tena sokoni iwapo zitarejeshwa kwa wakulima baada ya kukosa wanunuzi. Ngubiagai alionesha wasiwasi hiyo jana wakati wa kikao cha wadau wa korosho, ufuta na mbaazi ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, ambacho kilikuwa na lengo la kufanya tathimini ya ununuzi wa ufuta, mbaazi na maandalizi ya ununuzi wa korosho msimu wa 2020/2021. Ambapo kwa chama cha kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao utaanza 3.10.2020 na RUNALI 4.10.2020.Ngubiagai alionya kwamba korosho daraja la tatu zilizokosa wanunuzi na ambazo bado zipo kwenye ghala la Ilulu lililopo Nangurukuru, wilayani Kilwa zisipoondolewa na kutafutiwa utaratibu au zikirejeshwa kwa wakulima zitaingizwa sokoni msimu huu na kuharibu soko la zao hilo.Mbali na hofu ya kuingia sokoni na kuuzwa, DC huyo alisema korosho hizo zisipoondolewa zitasababisha nyingine zitakazo nunuliwa msimu huu zikose sehemu ya kuhifadhiwa. Kwani korosho zilizopo katika ghala hilo ni nyingi. Hata hivyo mashaka yake zitapelekwa wapi ambako hazitarejeshwa sokoni kwa mara nyingine.” Ndipo ni!ipo na mashaka korosho zile zinaweza kuingizwa sokoni tena. Lakini kuna changamoto ya vifungashio kuchelewa kuletwa. Yapo maeneo kule wilayani kwangu korosho zinavunwa mapema, kama kule Pande. Lakini vifungashio hadi sasa havijaletwa na mvua zikianza kunakuja mtihani tena kuhusu barabara,” alisema Ngubiagai.” Mheshimiwa mwenyekiti mbali na hayo kuna suala taasisi za fedha kushindwa kutekeleza ahadi kwa wakulima kwaajili ya pembejeo. Wakulima wanakamilisha na kutimiza vigezo na masharti wanayopewa na benki lakini hawakopeshwi. Napokea malalamiko mengi ya wakulima. Kama tumeamua kuwasaidia wakulima wetu lazima kila moja awe na komitimenti(Commitment/dhamira) ya kweli,” aliongeza kusema.Mkuu huyo wa wilaya pia alitoa wito vikao vya wadau ambavyo vinajumuisha wataalamu na watu wengine kutoka kwenye makundi na taasisi mbalimbali vitumike kubuni njia ya kuongezea thamani mazao badala ya kusafirisha na kuuza yakiwa ghafi. Kwani uzalishaji unaongezeka wakati solo la mazao ghafi linaendelea kuwa finyu.Aidha alitoa wito kwa mamlaka zinazohusika impatie kibali cha kuweka mizani nzuri na bora katika ghala la Nangurukuru ambalo linamilikiwa na Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS). Kwani mwendesha ghala hilo anauwezo wa kutatua changamoto ya mizani kwenye ghala hilo. Kwani ghala hilo linachangamoto ya mizani.Akijibu hofu ya korosho chafu kuingizwa sokoni, kaimu mkurugenzi wa masoko na ubora wa Bodi ya Korosho nchini(CBT), Domina Mkangala alisema ingawa sheria haijesma korosho za daraja hilo zifanywe nini lakini zikirejeshwa kwa wakulima kunauwezekano wa kurejeshwa tena sokoni.Kwakuzingatia ukweli huo alisema bodi hiyo itakaa ili kushauriana juu ya korosho hizo ambazo alisema zimeanza kuonekana na kupokewa kwa wingi msimu wa mwaka kutokana na ukaguzi mkubwa unaofanywa kudhibiti ubora. Akiweka wazi lengo lakikao hicho ni kuwaeleza wakulima kuwa korosho hizo hazifai.Alisema njia ambayo inaweza kutumika kudhibiti korosho hizo zisiingie tena sokoni ni kuziteketeza. Nibaada ya kuwasiliana na baraza la mazingira ( NEMC). Huku akiahidi hadi 25.09.2020 yatatolewa maamuzi yanini kifanyike kuhusu korosho hizo ambazo kwajina la utani kwa maeneo ya kanda ya Kusini zinajulikana kama GREDI KUTUPA.Kuhusu changamoto ya vifungashio viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya Lindi Mwambao na RUNALI walisema wamejipanga vema kwakuanza kukusanya korosho. Kwani vyama hivyo vinatarajia kupokea magunia leo tarehe 18.09.2020.,

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai ameonesha mashaka kuhusu hatima ya korosho daraja la tatu( Gredi kutupa) kurejea tena sokoni iwapo zitarejeshwa kwa wakulima baada ya kukosa wanunuzi. 

Ngubiagai alionesha wasiwasi hiyo jana wakati wa kikao cha wadau wa korosho, ufuta na mbaazi ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, ambacho kilikuwa na lengo la kufanya tathimini ya ununuzi wa ufuta, mbaazi na maandalizi ya ununuzi wa korosho msimu wa 2020/2021. Ambapo kwa chama cha kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao utaanza 3.10.2020 na RUNALI 4.10.2020.

Ngubiagai alionya kwamba korosho daraja la tatu zilizokosa wanunuzi na ambazo bado zipo kwenye ghala la Ilulu lililopo Nangurukuru, wilayani Kilwa zisipoondolewa na kutafutiwa utaratibu au zikirejeshwa kwa wakulima zitaingizwa sokoni msimu huu na kuharibu soko la zao hilo.

Mbali na hofu ya kuingia sokoni na kuuzwa, DC huyo alisema korosho hizo zisipoondolewa zitasababisha nyingine zitakazo nunuliwa msimu huu zikose sehemu ya kuhifadhiwa. Kwani korosho zilizopo katika ghala hilo ni nyingi. Hata hivyo mashaka yake zitapelekwa wapi ambako hazitarejeshwa sokoni kwa mara nyingine.

” Ndipo ni!ipo na mashaka korosho zile zinaweza kuingizwa sokoni tena. Lakini kuna changamoto ya vifungashio kuchelewa kuletwa. Yapo maeneo kule wilayani kwangu korosho zinavunwa mapema, kama kule Pande. Lakini vifungashio hadi sasa havijaletwa na mvua zikianza kunakuja mtihani tena kuhusu barabara,” alisema Ngubiagai.

” Mheshimiwa mwenyekiti mbali na hayo kuna suala taasisi za fedha kushindwa kutekeleza ahadi kwa wakulima kwaajili ya pembejeo. Wakulima wanakamilisha na kutimiza vigezo na masharti wanayopewa na benki lakini hawakopeshwi. Napokea malalamiko mengi ya wakulima. Kama tumeamua kuwasaidia wakulima wetu lazima kila moja awe na komitimenti(Commitment/dhamira) ya kweli,” aliongeza kusema.

Mkuu huyo wa wilaya pia alitoa wito vikao vya wadau ambavyo vinajumuisha wataalamu na watu wengine kutoka kwenye makundi na taasisi mbalimbali vitumike kubuni njia ya kuongezea thamani mazao badala ya kusafirisha na kuuza yakiwa ghafi. Kwani uzalishaji unaongezeka wakati solo la mazao ghafi linaendelea kuwa finyu.

Aidha alitoa wito kwa mamlaka zinazohusika impatie kibali cha kuweka mizani nzuri na bora katika ghala la Nangurukuru ambalo linamilikiwa na Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS). Kwani mwendesha ghala hilo anauwezo wa kutatua changamoto ya mizani kwenye ghala hilo. Kwani ghala hilo linachangamoto ya mizani.

Akijibu hofu ya korosho chafu kuingizwa sokoni, kaimu mkurugenzi wa masoko na ubora wa Bodi ya Korosho nchini(CBT), Domina Mkangala alisema ingawa sheria haijesma korosho za daraja hilo zifanywe nini lakini zikirejeshwa kwa wakulima kunauwezekano wa kurejeshwa tena sokoni.

Kwakuzingatia ukweli huo alisema bodi hiyo itakaa ili kushauriana juu ya korosho hizo ambazo alisema zimeanza kuonekana na kupokewa kwa wingi msimu wa mwaka kutokana na ukaguzi mkubwa unaofanywa kudhibiti ubora. Akiweka wazi lengo lakikao hicho ni kuwaeleza wakulima kuwa korosho hizo hazifai.

Alisema njia ambayo inaweza kutumika kudhibiti korosho hizo zisiingie tena sokoni ni kuziteketeza. Nibaada ya kuwasiliana na baraza la mazingira ( NEMC). Huku akiahidi hadi 25.09.2020 yatatolewa maamuzi yanini kifanyike kuhusu korosho hizo ambazo kwajina la utani kwa maeneo ya kanda ya Kusini zinajulikana kama GREDI KUTUPA.

Kuhusu changamoto ya vifungashio viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya Lindi Mwambao na RUNALI walisema wamejipanga vema kwakuanza kukusanya korosho. Kwani vyama hivyo vinatarajia kupokea magunia leo tarehe 18.09.2020.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *